Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: AZAM FC YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA MNYAMA (SIMBA SC) YAKUBALI KICHAPO
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Jumamosi ya Septemba 17, 2016  Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea tena   kwa michezo sita ku...
Jumamosi ya Septemba 17, 2016 Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea tena  kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja sita tofauti, moja kati ya mchezo uliochezwa ni Azam FC waliwakaribisha Simba katika dimba Uhuru Dar es Salaam, katika mchezo ambao kila mmoja alikuwa anawania kupata ushindi ili apate nafasi ya kuongoza Ligi hiyo.

Huu ulikuwa ni mchezo unaozikutanisha timu ambazo zote zilikuwa na point 10 na wastani wa magoli ya kufunga na kushinda walikuwa wapo sawa, haukuwa mchezo rahisi kuona timu ikiruhusu kufungwa kwani hadi dakika ya 45 za kwanza zinamalizika walikuwa 0-0.

Kipindi cha pili dakika ya 67 Simba wakabadili ubao wa matokeo na kuufanya usomeke 1-0 baada ya Shiza Kichuya kufunga goli la ushindi kwa shuti kali lililomshinda golikipa wa Azam FC Aishi Manula.


Simba sasa atashuka dimbani Septemba 24 kucheza dhidi ya Majimaji katika uwanja wa Uhuru, wakati Azam FC watakuwa Mtwara kucheza na Ndanda FC.

MATOKEO YA MICHEZO YA LEO VPL
VPL Result
______________________________________
ULIPITWA NA HII YA NISHA KUCHORA TATOO YA BARAKA? CHEKI HAPA

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top