Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: ANDREY COUNTINHO AYAZUNGUMZA HAYA MARA BAADA YA KUREJEA YANGA SC
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Andrey Coutinho yupo nchini kwa lengo kuu moja tu kuja kujaribu bahati yake ya kuitumikia Yanga S...
Andrey Coutinho yupo nchini kwa lengo kuu moja tu kuja kujaribu bahati yake ya kuitumikia Yanga SC kwa mara nyingine tena. .
Andrey Coutinho
"Kama ukisikia nimerudi katika ligi kuu Tanzania basi jua nimerudi katika klabu nnayoipenda Yanga, siwezi kuichezea timu yoyote zaidi ya Yanga . . Nimegundua soka la Yanga linahitaji nguvu na akili, sasa nipo kamili!

"Ntasubiri hapa kwa siku 5 kuangalia uwezekano wa kujisajili Yanga, nimepanga kesho kuwepo uwanjani kuwasalimia mashabiki na wachezaji wenzangu" alimalizia raia huyo wa Brazil.
Andrey Coutinho
Coutinho amemaliza mkataba wake katika klabu ya Rakhine United FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Myanmar barani Asia akifanikiwa kutupia wavuni magoli 10.

Haya ya Coutinho yakiendelea winga Mtanzania Mrisho Ngassa anaendelea kusotea ombi lake mara baada ya kuomba kurudi Yanga ili amalizie soka lake kiheshima katika klabu aipendayo.

HAPA COUTINHO PALE NGASSA, YUPI MMOJA WAO KATI YAO UNGEPENDA AREJESHWE YANGA?
Chanzo: Naipenda Yanga


___________________________________________________
ITAZAME HAPA VIDEO MPYA YA MALAIKA - RARUA KISHA TOA MAONI YAKO

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top