Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: ACTION AID YABAINISHA CHANGAMOTO ZA SEKTA YA ELIMU KILWA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Na.Ahmad Mmow, Kilwa. Kiwango kidogo cha ufaulu katika shule za msingi na sekondari Wilayani Kilw...
Na.Ahmad Mmow, Kilwa.
Kiwango kidogo cha ufaulu katika shule za msingi na sekondari Wilayani Kilwa mkoani Lindi kimetajwa kusababishwa na changamoto nyingi katika sekta ya elimu wilayani humo.
Wanafunzi
Hayo yalielezwa jana mjini Kilwa masoko, na mtafiti wa shirika la Action aid, Jacob Kateri wakati anawasilisha ripoti ya utafiti wa awali wa mpango wa maendeleo ya elimu katika wilaya hiyo.

Kupitia mradi wa uwezeshaji elimu kwa kutumia rasilimali za ndani ya nchi.

Akisoma ripoti hiyo kwa wadau wa elimu wa wilaya hiyo, Kateri alisema katika utafiti huo uliowahusisha wadau waelimu ikiwawamo, walimu, wazazi na wanafunzi. 

Imebainika kwamba sekta ya elimu wilayani humo inachangamoto nyingi zinazohitaji kufanyiwa kazi na serikali kwa kushirikiana na jamii, ili kiwango cha utoaji elimu kiboreke na kuongeza kiwango cha ufaulu.

Kateri ambae shirika lake lilifanya utafiti huo kwa kushirikiana na mtandao wa mashirika yasio ya kiserikali ya wilaya ya Kilwa(KINGONET) alizitaja changamoto hizo kuwa ni wazazi kutojua umuhimu wa elimu, umasikini na kilimo cha kuhamahama.

Alisema umasikini wakipato kwa wazazi wilayani humo unasababisha washindwe kuwapatia watoto wao mahitaji muhimu na yalazima.

Ambapo baadhi ya wazazi wanawatumia watoto katika shughuli na kazi za uzalishaji mali badala ya kuwahimiza waende shuleni.

Alisema licha ya umasikini lakini pia jamii wilayani humo haitambui umuhimu wa elimu hivyo kushindwa kushiriki na kuchangia kuinua kiwango cha elimu. Ikiwamo kujitolea kujenga nyumba za walimu, vyoo na madarasa.
"Kilimo cha kuhamahama pia kinasababisha wazazi kushindwa kuwasimamia kwa karibu watoto wao, na wengine wanahama nao nakusababisha washindwe kuhudhuria shuleni," alisema Kateri.

Kateri alibainisha kuwa kiwango cha watoto kuacha shule ni 3.5% ya watoto wote walioandikishwa. Kati yao wavulana wakiwa 4.2% na wasichana 2.3%. 

Ambapo katika utafiti huo imebainika katika shule 15 zilizohusishwa na utafiti huo imebainika kuwa ingawa uwiano unatakiwa tundu moja kutumiwa na wavulana 20 na 25 kwa wanawake, lakini wilayani humo uwiano ni tundu moja kwa wavulana 61, na 55 kwa wasichana walio andikishwa. Kati yao wavulana wakiwa 4.2% na wasichana 2.3%.

Ambapo imeelezwa wakati wavulana wakiacha shule kwasababu ya kufanya biashara kwenye vituo vya mabasi na shuguli za uvuvi. Wasichana kwa upande wao wanaacha shule kutokana na ushawishi wa wazazi kuwatumia kwa kazi ndani na ajira za kazi ndani mijini.

Kateri aliendelea kusema upungufu wa walimu katika wilaya hiyo ni mkubwa kiasi cha kusababisha baadhi ya shule za msingi kuwa na wastani wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 81.

Aidha Kateri alibainisha tatizo la uhaba wa vyoo ambao unasababisha wanafunzi kukosa utulivu kutokana na kutokuwa na uhakika wa kwenda kujisaidia wawapo shuleni. 

Kuhusu uandikishaji wawatoto katika madarasa yote, mtafiti huyo alisema kiwango cha uandikishaji kimeongezeka.

Akibainisha kwamba ongezeko la uandikishaji toka mwaka 2015 na mwaka 2016 ni 7.8% bila kujali jinsia. Ambapo uandikishaji kwa darasa la kwanza umeongezeka kwa 50% kwa mwaka 2016, wavulana walioandikishwa wakiwa 61% na wasichana 37%.

Hata hivyo alisema watoto wa umri wa kuwa shuleni ambao bado wapo nje ya shule ni 3.6% ya wanafunzi wote.

Huku 3.5% wakiwa wasichana na 3.6% ni wavulana.
"Shule zinazokadiriwa kuwa na watoto wengi wa umri wa kuwa shuleni ambao wapo nje ya shule ni Lihimalyao, Nandembo na Mingumbi.

Hata hivyo adhabu ya viboko inaongoza kwani kati ya shule 15, shule 14 zimesema ni suala la kawaida, huku ikifuatiwa na ukatili wa kimwili ambopo shule nne wamesema nikawaida" ukatili wa kingono nao umetajwa katika shule tatu, moja ikisema umetokea mara chache na kumi zimesema haujatokea,"  alisema Kateri.

Kwa upande wake mkuu wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai licha ya kuipongeza halmashauri ya wilaya kupitia idara ya elimu ya shule ya msingi kwa kupandisha kiwango cha ufaulu wilayani humo kutoka 33% mwaka 2013 hadi kufikia 56% mwaka jana.

Alisema tatizo la upungufu wa walimu nikubwa ambapo wilaya hiyo inaupungufu wa walimu 307 wa shule za msingi.

Ngubiagai aliwataka walimu kuishi katika vituo vyao vyakazi badala ya nje ya vituo vyao. Huku akihaidi kuwazawadia baiskeli walimu ambao shule zao zitakuwa na matokeo mazuri ya ufaulu.MWISHO.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top