Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AWATAKA POLISI KUWEKA ULINZI WA KUTOSHA KWENYE BANDARI BUBU MKOANI LINDI.
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi,  Mwigulu Nchemba. Na. Mwandishi Wetu, Lindi Waziri wa mam...
Mwigulu Nchemba
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba.

Na. Mwandishi Wetu, Lindi
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba, amevitaka vikosi vya ulinzi na usalama, katika mikoa ya Lindi na Mtwara, kuhakikisha wanapambana na kuweka ulinzi wa kutosha sehemu zote za bandari bubu ili kuepusha wale wote wanaotumia bandari hizo kusafirisha madawa ya kulevya.

Waziri huyo wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba ameyasema hayo mkoani Lindi wakati akiongea na vikosi vya ulinzi na usalama, ikiwemo Jeshi la Polisi, magereza, uhamiaji pamoja na jeshi la zimamoto huku akisisitiza kuweka ulinzi wa kutosha na endelevu katika bandari bubu zote zilizopo mikoa ya Lindi na Mtwara, ambazo zimekuwa zikitumika kwa kiasi kikubwa kwa kupitishwa madawa ya kulevya.

Hata hivyo waziri Nchemba, akavitaka vikosi hivyo vya ulinzi na usalama kulinda heshima ya taasisi yao ikiwemo kutoa haki kwa wanyonge wanapopeleka kesi katika vyombo hivyo ambavyo vimekuwa vikitegemewa kwa kiasi kibwa katika kulinda raia na mali zao.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top