Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: WAZIRI GOERGE SIMBACHAWENE ATAKA RASILIMALI ZIWANUFAISHE WANANCHI
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmed Mmow, Lindi Halmashauri ya wilaya Kilwa mkoani Lindi imetakiwa kusimamia na kupiti...
Na.Ahmed Mmow, Lindi
Halmashauri ya wilaya Kilwa mkoani Lindi imetakiwa kusimamia na kupitia upya mapato ya ushuru unaotokana na gesi asilia ili yaboreshe huduma za kijamii.
Goerge Simbachawene
Agizo hilo limetolewa katika kijiji cha Songosongo, na waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Goerge Simbachawene alipokuwa anazungumza na wakazi wa kijiji hicho kilichopo wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi.

Simbachawene alisema kama halmashauri itapanga na kutenga kiasi cha fedha kinachotokana na gesi asilia inayovunwa katika kijiji hicho kwa ajili ya maendeleo ya maisha ya wananchi ni lazima itambue kuwa kuna watu wanaosaidia kutunza na kulinda miundombinu.


Hivyo wanatakiwa wajione ni sehemu ya maendeleo yanayopatikana kutoka kwenye raslimali zilizopo.

Pia waziri Simbachawene amewataka wananchi wa kijiji hicho kutumia gesi hiyo kwa ajili ya kujieletea maendeleo kwa kufanya shughuli za halali na kuwafichua watu watakao tumia gesi hiyo kwa kupitisha biashara za magendo.
"Mnayo haki ya kunufaika na gesi iliyogunduliwa katika kijiji hiki, lakini pia mnawajibu wakuwafichua wanataka kutumia mwanya huo kupitishia na kutoshea biashara haramu na magendo," alisisitiza Simba Chawene.
Awali mkurugenzi msaidizi uendeshaji wa miundombinu, mhandisi Gilbert Mwonga, alisema ujenzi wa mradi wa gesi asilia ya Songosongo ambao ulianza kujengwa mwaka 2004 kwa ushirikiano baina ya benki ya dunia na serikali ya Tanzanzia kwa gharama ya shilingi bilioni 3.3 upo kwenye kipindi cha matazamio.

Mwonga alibainisha kuwa kukamilika kwa mradi wa gesi hiyo utakuwa na manufaa ya kiuchumi na kijamii kwa wakazi wa kisiwa cha Songosongo,wilaya Kilwa na taifa kwa jumla.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top