Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: WANENE ENTERTAINMENT WAMWAGA MBOGA BAADA YA HANSCANA KUMWAGA UGALI
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Baada ya muongozaji wa video nchini Hanscana kujitoa kwenye kampuni iliyokuwa ikimsamimia, Wanene ...
Baada ya muongozaji wa video nchini Hanscana kujitoa kwenye kampuni iliyokuwa ikimsamimia,Wanene Entertainment,kwa upande wao (Wanene) wamefunguka na kusema kuwa hakuna ugomvi kati yao na Hanscana bali tu walishindwa kukubaliana kwenye vitu kadhaa.
Hanscana
Akiongea kwenye mahojiano na radio 5, Gentriez ambaye ni mmoja kati ya watu wa ndani wa kampuni hiyo amesema kuwa Hanscanah alisema anataka atimiziwe vitu kadhaa la sivyo angevunja mkataba na ndichi kilichotokea.
Hanscana
“Ni kweli Hanscana hayupo wanene Entertainment, hajafukuzwa lakini amejiuzulu kutokana na mkataba aliopewa na kampuni hakuwa ameuridhia.Yeye alitaka mahitaji fulani kwa kampuni kama Red camera,ili afanye kazi kwa ufanisi zaidi,lakini kampuni ilimwambia asubiri kidogo atumie zilizopo halafu mbeleni atapata hiyo camera maana ni hela ndefu kidogo,pia alikuwa analalamika kuwa kampuni imewekeza hela nyingi kwenye audio kuliko video,n hivyo tu hakuna bifu yoyote” alieleza Gentriez

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top