Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: WANAOWAPELEKA WATOTO JANDONI KIPINDI CHA MASOMO KUKIONA CHA MTEMA KUNI.
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Rukia Muwango Na. Ahmad Mmow, Nachingwea Serikali Wilayani Nach...
Rukia Muwango
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Rukia Muwango

Na. Ahmad Mmow, Nachingwea
Serikali Wilayani Nachingwea imesema haitawavumilia na itawachukulia hatua kali wazazi wanaowapeleka jandoni watoto wao katika kipindi cha masomo.

Onyo hilo lietolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Rukia Muwango wakati wa hafla ya kukabidhiwa madawati 737 kutoka kwa mbunge wa jimbo la Nachingwea, Hassan Masala.

Muwango alisema juhudi za serikali zitakuwa na matokeo mazuri iwapo wazazi na walezi watatambua wajibu wao. Ikiwamo kuhakikisha watoto wao wanahudhuria shuleni siku zote bila kukosa.

Alibainisha kwamba miongoni mwa sababu zinazochangia baadhi ya watoto kuwa na ufaulu mdogo kwenye mitihani hasa kwa shule za msingi zilizopo Wilayani humu ni utoro ambapo shughuli na sherehe za jando maarufu kwa jina la unyago alizitaja kuwa nimiongoni mwa sababu zinazo sababisha utoro huo.

Alisema serikali imejitahidi kuandaa mazingira mazuri kwa watoto kupata elimu bila ya shida ikiwemo kumaliza tatizo la madawati na elimu kutolewa bure.

Hivyo hatakubali kuona nia ya serikali na ndoto za watoto kuwa na viwango bora vya elimu zinazimwa na wazazi na walezi wasio na uchungu na elimu.
"Serikali inaamini  na kuheshimu mila na Tamaduni zetu, hata hivyo mzazi au mlezi atakaempeleka mwanafunzi jandoni kipindi cha masomo sitasita kumchukulia hatua za kisheria." alisema Muwango.

Katika hali iliyoonesha kuwa mwakilishi huyo wa Rais ngazi ya Wilaya hana masihara kuhusu onyo hilo alisema amemuagiza mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo awasiliane na ofisa elimu afuatilie na kuwajua watoto ambao hawajahudhuria shuleni katika kipindi hiki ambacho shughuli za unyago zimeshika kasi katika wilaya hii ili wazazi wao wachukuliwe hatua za kisheria bila kuchelewa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top