Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: WANANCHI WAONYWA KUHUSIANA NA MATAMKO YANAYOTOLEWA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Nachingwea Wananchi wameombwa kutafakari kabla ya kuyafanyia kazi matamko na maagi...
Na. Ahmad Mmow, Nachingwea
Wananchi wameombwa kutafakari kabla ya kuyafanyia kazi matamko na maagizo ya viongozi wa vyama vya siasa dhidi yao.
Albert Mnali
Wito huo umetolewa leo na mwenyekiti wa kituo cha demokrasia wa wilaya ya nachingwea Albert Mnali wakati wa kikao cha pili cha kituo hicho kilichofanyika mjini Nachingwea. 

Mnali ambae pia ni mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Nachingwea alisema wananchi na viongozi wa ngazi za chini wa vyama vya siasa hawana budi kutafakari matamko na maagizo ya viongozi wa juu wa vyama vya siasa kabla ya kufanyia kazi.

Kwa madai kwamba baadhi ya maagizo na matamko hayo hayana mwisho mwema katika kudumisha amani na utulivu uliopo hapa nchini. alisema kabla ya kupokea na kufanyia kazi ni vizuri waanze kuangalia na kupima yanamanufaa gani kwao, ustawi na maendeleo ya nchi.

Alibainisha kuwa katika nchi za watu wastaharabu, ikiwamo nchi hiiambayo wananchi wake wamezoeaamani, njia kubwa ya kumaliza tofauti katika jamii ni majadiliano.
"Nchi hii ni moja na watu wake ni wamoja, tunatakiwa kuendelea kuwa hivyo, tusikubali kutumiwa kwa maslahi ya watu kutokana na tofauti ambazo zinaweza kutatuliwa kwa njia ya majadiliano," alisema Mnali.

Aidha Mwenyekiti huyo aliwahi kuwa mkuu wa Wilaya katika Wilaya mbalimbali hapa nchini alitoa wito kwa jeshi la polisi kujenga utamaduni wa kutoa elimu kwa raia badala ya kutumia nguvu.

Akibainisha kwamba wananchi wanatakiwa kuelimishwa na kuelezwa kwanza madhara na hata makosa yao badala ya kuanza kuwatisha.
"Sina maana muwaache wanavunja sheria , bali toeni elimu kabla ya kutumia nguvu, maana hata polisi jamii wanatishawatu," alisisitiza Mnali.

Nae mwakilishi wa polisi kamanda wa polisi wa wilaya ya Nachingwea kwenye kikao hicho mkaguzi wa polisi Ombeni Nko alisema wanasiasa wanawajibu wa kutoa elimu kwa wananchi ili watambue umuhimu wa kushirikiana na jeshi hilo.

Akibainisha kwamba mahali ambapo hapana amani na usalama hakuna maendeleo kwa sababu wafanyabiashara wanapenda kufanyabiashara mahali ambapo wanauhakika wa usalama wao na mali zao.

Kikao hicho ni cha pili kufanyika ambacho kilifuatia kikao cha awali kilichofanyika mwezi juni mwaka huu, ambapo uzinduzi rasmi wa kituo hicho cha demokrasia (TCD) wilayani Nachingwea unatarajiwa kufanyika mwezi oktobamwaka huu.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top