Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: WANAFUNZI WANUSURIKA KIFO WAKIWA SAFARINI KUELEKEA KATIKA MAONYESHO YA NANE NANE MKOANI LINDI
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Lindi. Wanafunzi 90 wa shule ya Sekondari Mnara Rondo Jimbo la Mtama mkoani L...
Lindiyetu News
Na. Ahmad Mmow, Lindi.
Wanafunzi 90 wa shule ya Sekondari Mnara Rondo Jimbo la Mtama mkoani Lindi wamenusurika kufa baada ya Lori walilokuwa wakisafiria kuelekea kwenye Maonesho ya nanenane yanayofanyika viwanja vya Ngongo manispaa ya Lindi, kupinduka.

Akielezea kuhusu tukio hilo, Mwalimu Maulidi Imili alisema lilitokea majira ya saa tano asubuhi katika kijiji cha Rutamba walipokuwa wanatoka Shule ya Sekondari Mnara akiwa na wanafunzi hao waliokuwa wana kwenda kwenye maonesho hayo ili kuangalia na kujifunza mambo mbalimbali yatayowasaidia kuongeza uelewa katika masomo.

Maulidi alisema baada ya kufika Rutamba dereva alijaribu kulikwepa Korongo lililopo barabarani, ndipo lori hilo likayumba kulia na kushoto nakusababisha bomba walizokuwa wameshikilia zikatike na kuwamwaga.

Kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Sokoine Msafiri Regnald amekiri kupokea wanafunzi majeruhi 10 ambao kati yao wanne hali zao mbaya kutokana kuvunjika maeneo mbalimbali ya viongo vyao.

Nae kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa wanafunzi 80 kati ya waliopata ajili hawakuumia na 10 walioumia wanaendelea kupata matibabu katika hospitali ya Mkoa ya Sokoine.

Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi ameuagiza uongozi wa hospitali ya rufaa ya Sokoine kuzingatia maadili ya kazi yao.

Agizo hilo amelitoa wakati alipokwenda kuwaona na kuwajulia hali wanafunzi hao. Nibaada ya kubaini majeruhi hao kukosa matibabu kwa zaidi ya saa saba tangu wafikishwe katika hospitali hiyo. Huku kaimu mganga mkuu Regnald, akisema wanafunzi hao walichelewa kupata matibabu kutokana na upungufu wa madaktari kwani hospitali hiyo ina Daktari mmoja ambaye muda huo alikuwa anawahudumia wagonjwa wengine katika wodi nyingine.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top