Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: WAKUU WA WILAYA WAPEWA SIKU SABA KUHAKIKI MADAWATI, VYETI FEKI NA WANAFUNZI HEWA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Serikali mkoani Mbeya imewaagiza wakuu wa wilaya zote kuhakikisha wanawasilisha fomu za taarifa za...
Serikali mkoani Mbeya imewaagiza wakuu wa wilaya zote kuhakikisha wanawasilisha fomu za taarifa za Utengenezaji na ugawaji wa madawati kwenye shule zote ndani ya siku saba lengo likiwa ni kupata uhakika wa utekelezaji wa Agizo la Rais Dkt. Magufuli.
Amos Makala
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala amesema lengo la agizo hilo ni kuepuka taarifa za Madawati Hewa zinazoweza kusababisha mkoa kuamini kuwa tatizo la uhaba wa madawati limemalizika kumbe si kweli.

Katika kikao cha kazi kilichofanyika jana na kuhudhuriwa na wakuu wa wilaya za mkoani Mbeya,wakurugenzi na makatibu Tawala, Makalla ameagizo wakuu wa wilaya kupita kila shule kufanya uhakiki wa utekelezaji wa agizo la rais na ifikapo Agosti 11 mwaka huu wawasilishe fomu itakayokuwa imewekwa saini na mkurugenzi wa halmashauri na afisa elimu wa wilaya husika juu ya uhakiki wa madawati.

Amesema upo uwezekano mkubwa wa baadhi ya maeneo kuwa na madawati mengi yaliyotengenezwa kwakuwa wapo baadhi ya viongozi walipoambiwa wafanye utambuzi wa dawati zinazohitajika walizidisha idadi wakijua serikali italeta fedha hivyo ikawalazimu kutengeneza madawati mengi zaidi ya uhalisia uliokuwepo.

Amesema wapo pia ambao ama kwa kuona watakuwa wanajifichia uovu wanaweza kuwa walipunguza idadi ya madawati yaliyokuwa yakihitajika hivyo mkoa unaweza ukaingia mkenge iwapo utatangaza kumaliza uhaba wa madawati lakini siku chache ikabainika kuna shule wanafunzi wanakaa chini.

Makalla alisema amelazimika kuweka utaratibu huo baada ya kutembelea baadhi ya halmashauri na kubaini kuwepo kwa manung’uniko aliyosema yatamalizika baada ya uhakiki huo kufanyika kwenye maeneo yote.

Mkuu huyo wa mkoa ameagiza pia uongozi kuendelea kufanyia kazi agizo la ofisi ya Utumishi wa umma la ukaguzi wa vyeti vya wafanyakazi pamoja na agizo la Rais la kubaini wanafunzi hewa mashuleni.*****************************************************

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top