Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: VYAMA VYA BODABODA VYAUNGANA NA MBOWE KUHUSU UKUTA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Katibu wa Chama cha Waendesha Bodabaoda, Oscar Wiluye (katikati) akisisitiza jambo wakati wa Mku...
Oscar Wiluye
Katibu wa Chama cha Waendesha Bodabaoda, Oscar Wiluye (katikati) akisisitiza jambo wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) leo hii.

WAKATI Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akitoa tamko lake la kuahirisha maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika nchi nzima chini ya wito wa Ukuta kesho Septemba Mosi, viongozi wa vyama vya waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam, vimeungana naye kwa kusema kuwa kama maandamano hayo yangelifanyika wao wasingeshiriki.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Bodaboda, Almano Leonard, alisema kuwa ilikuwa marufuku kwa wanachama wao kujihusisha na masuala mazima ya kisiasa yakiwemo maandamano hususani siku iliyokuwa imepangwa ya kesho.

Alisema kuwa isingewezekana mwanachama yeyote kubeba abiria aliyevalia sare ya chama chochote kwani hatua kali kwa ambaye angelithubutu zingelichukuliwa na viongozi wao wa wilaya.

Mbowe ameahirisha maandamano hayo kwa muda wa mwezi mmoja ili kutoa fursa kwa viongozi wa dini kutafuta muafaka wa majadiliano na serikali.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top