Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: VODACOM YAKABIDHI VIFAA KWA TIMU ZINAZOSHIRIKI LIGI KUU YA VODACOM MSIMU WA 2016/2017
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Timu zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, Zimekabidhiwa vifaa mbalimbali na mdhamini mk...
Timu zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, Zimekabidhiwa vifaa mbalimbali na mdhamini mkuu wa ligi hiyo Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo vina thamani ya shilingi milioni 514,208,400/=
Jezi mpya ligi ya vpl 2016/2017
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nandi Mwiyombella(mwenye miwani)na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa klabu mbalimbali wakati wa hafla ya ukabidhi vifaa kwa timu za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi hiyo jijini Dar es Salaam leo.

Akikabidhi vifaa hivyo jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo,Nandi Mwiyombella ,alisema kuwa kwa mara nyingine tena katika kuhakikisha ligi ya soka nchini inaenda vizuri Vodacom inakabidhi vifaa mbalimbali vya ligi ambavyo ni jezi mbalimbali, viatu vya mazoezi na mechi, soksi, vilinda ugoko, nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves na vifaa vingine vingi vinavyohitajika.
Nandi Mwiyombella
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nandi Mwiyombella akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu zitakazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara,Jijini Dar es Salaam.

“Tunajisikia furaha kukabidhi vifaa hivi siku ya leo tukiwa tunatekeleza matakwa ya mkataba wa udhamini, ni imani yetu kwamba timu zitakazoshiriki ligi zimejiandaa vya kutosha kwa msimu mpya wa ligi wa 2016/2017”
Alisema Mwiyombella.

Mwiyombella alisema Vodacom inaendelea kudhamini ligi kuu kwa sababu soka ni mchezo unaopendwa sana hapa nyumbani ukiwa na washabiki wengi hivyo inapenda kuona wananchi ambao baadhi yao ni wateja wake wanapata burudani ya mchezo waupendao pia siku zote inaamini kuwa michezo ni ajira kubwa duniani kote, ikiendelezwa inaweza kubadilisha maisha ya watu wengi na taifa kunufaika kwa mapato makubwa ya kodi kutoka katika sekta hii.
Boniface Wambura
Ofisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura akitoa neno la shukurani kwenye hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu zitakazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara,Hafla hiyo iliandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi hiyo Vodacom Tanzania jijini Dar es Salaam.

Aliwataka wadhamini wengine kujitokeza ili kuboresha zaidi ligi ya Tanzania na kuongeza maslahi kwa wachezaji wanaoshiriki katika ligi “Tukiunganisha nguvu timu zetu zinaweza kuwa na wachezaji wa kimataifa pia ni muhimu kwa wadau mbalimbali kuanza kuwekeza katika timu za vijana chipukizi kwa kuwa vipaji vinaanzia ngazi ya chini ambako vinapaswa kuibuliwa na kuendelezwa ”Alisema Mwiyombella.
Jezi mpya ligi ya vpl 2016/2017
JEZI ZA TIMU YA YANGA KWA MSIMU WA 2016/2017

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura aliishukuru hiyo, na kuzitaka klabu zinazoshiriki ligi hiyo kuheshimu chapa ya mdhamini wakati wote wa mechi za ligi.
“Ninatoa mwito kwa klabu zote kutumia jezi zenye nembo ya mdhamini mkuu katika kuhakikisha ligi inafanikiwa kama inavyotakiwa,” alisema.
Jezi mpya ligi ya vpl 2016/2017
JEZI ZA TIMU YA SIMBA KWA MSIMU WA 2016/2017

Aliongeza kuwa TFF isingependa kutumia kanuni na sheria kuadhibu klabu inayokwenda kinyume, bali kila klabu izingatie masharti ya mdhamini kama ambavyo anavyotimiza haki yake ya kuwapatia vifaa.
Jezi mpya ligi ya vpl 2016/2017
JEZI ZA TIMU YA TANZANIA PRISON KWA MSIMU WA 2016/2017

Alisema ligi ya mwaka huu itakuwa bora kutokana na maandalizi yote kukamilika mapema pia timu zitazoshiriki zimejiandaa vya kutosha kuhakikisha ligi inakuwa na msisimko na ushindani mkubwa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top