Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: UVCCM KUFANYA MAANDAMANO AGOSTI 31, HII HAPA SABABU YA MAANDAMANO HAYO
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Shaka Hamdu Shaka Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Na. Mwandishi Wetu,...
Shaka Hamdu Shaka
Shaka Hamdu Shaka Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM)

Na. Mwandishi Wetu, Dar es salaam.
Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikitarajia kufanya maandamano na mikutano ya hadhara nchini nzima kuanzia tarehe 1 septemba mwaka huu , kwa kile wanachodai kupinga vitendo vya ukandamizaji wa vyama vya upinzani vinavyofanywa na Rais John Magufuli.

Ambapo Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Umetangaza kufanya maandaamano nchini nzima siku ya tarehe 31 ya mwezi huu kwa ajili ya kumpongeza Rais Magufuli kwa kile wanachokisema hatua “anazochukua Rais huyo kuinua uchumi”.
Rais John Magufuli
Shaka Hamdu Shaka ambaye ni Katibu wa Umoja huo ameyatangaza maandamamo hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari amesema tayari wamemuandikia barua mkuu wa jeshi la Polisi nchini (IGP)Ernest Mangu wakitaka kuwaruhusu wafanye maandamamo wanayodai ni ya amani.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top