Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: TUNDU LISSU AMKOSOA TENA RAIS MAGUFULI KWA UAMUZI WAKE HUU JUU YA WAWEKEZAJI WA MADINI NCHINI
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Katika hotuba yake ya kumalizia ziara yake akiwa Mkoani Geita Kata ya Kotoro Rais Magufuli alinukul...
Katika hotuba yake ya kumalizia ziara yake akiwa Mkoani Geita Kata ya Kotoro Rais Magufuli alinukuliwa akisema kuwa ni marufuku kusafirisha mchanga wenye madini nje ya nchi.
Rais Magufuli
Zaidi ya dhahabu, mgodi wa Bulyanhulu unazalisha pia madini ya fedha (silver), cobalt, copper na cadmium (ya mwisho kama sikosei!). Bulyanhulu ni mgodi pekee nchini wenye madini yote hayo na mchanga unaosafirishwa nje unatoka Bulyanhulu. Madini yote hayo, kwa mujibu wa Sheria ya Madini na Mikataba ya Uendelezaji Madini (MDAs) waliyopewa na Rais Benjamini Mkapa na kurudiwa na Jakaya Kikwete, ni mali ya wawekezaji ambapo mgodi huo unafanya smelting ya dhahabu tu (takriban 70% ya processing yote). 30% iliyobaki inafanyikia Japan ambayo ina hiyo ambapo kuna mitambo ya kumalizia kuchambua madini mengine yaliyobaki.

Kwa mujibu wa Mbunge Tundu Lissu amesema Rais Magufuli angewaelekeza wawekezaji wajenge kwanza huo mtambo ndani ya nchi kabla ya kupiga marufuku kusafirishwa mchanga. Kwa kuzingatia kwamba wawekezaji hawa wanalindwa kisheria na kimkataba. Au angeamuru urekebishwaji wa sheria ili kufanya mchakato wote ufanyike ndani ya nchi.
Lissu
Lissu amesema kuwa kutofanya hivo matokeo yake atagombana na wawekezaji na serikali zao na huenda wakapeleka mashitaka kwenye mahakama za kimataifa ambazo Marais wastaafu Mkapa na Kikwete walizikubali kuwa ndio mahakama za migogoro kati ya Tanzania na wawekezaji wetu.

Rais Evo Morales wa Bolivia alikuwa na mikataba ya Madini kama ya Tanzania alipochaguliwa mwezi Desemba ya 2006 kitu cha kwanza alichofanya ni kuiondoa Bolivia kwenye MIGA Convention na kwenye bilateral investment treaties (BITs) zilizokuwa zinalazimisha international arbitration kwenye migogoro ya uwezekaji. Baada ya hapo ndio akabadilisha sheria na mikataba ya uwekezaji iliyoipa Bolivia sehemu kubwa ya umilikaji wa gesi na mafuta ya nchi yake.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top