Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: TFS YAZIDI KUUNGA MKONO DHAMIRA YA RAIS KUMALIZA TATIZO LA MADAWATI
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Na Ahmad Mmow, Nachingwea. Wakala wa huduma za misitu(TFS) umeendelea kuunga mkono dhamira ya Rais...
Na Ahmad Mmow, Nachingwea.
Wakala wa huduma za misitu(TFS) umeendelea kuunga mkono dhamira ya Rais Dkt John Magufuli ya kumaliza tatizo la madawati katika shule za serikali.
madawati
Baada ya TFS wilayani Nachingwea mkoani Lindi, juzi kukabidhi madawati 80 kwa mkuu wa wilaya hiyo Zainab Mwango. Akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika mjini Nachingwea, meneja wa TFS wa wilaya hiyo, Togolai Tindikali, alisema msaada huo ni utekelezaji wa agizo la mtendaji mkuu wa TFS lilotaka kila wilaya kuchangia idadi hiyo ya madawati.

Huku akiishukuru ofisi ya mkuu wa wilaya na halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kwa ushirikiano uliosaidia kufanikisha utengenezaji wa madawati hayo. Aidha meneja huyo alizitaja changamoto zinazoikabili sekta ya misitu. Ikiwamo kiliomo cha kuhamahama, uchomaji moto misitu na uvunaji wa kutumia misumeno ya moto.

Alisema kilimo cha kuhamahama na uchomaji misitu ni tatizo linalotishia uwepo wa misitu katika kipindi kifupi kijacho. Iwapo jamii haitabadilika na kutambua umuhimu na thamani ya misitu katika maisha yake. 

Alisema wakulima wengi wamekuwa na tabia ya kuhama kila mwaka kwa kuacha mashamba ya awali nakuanzisha mapya.

Hali ambayo inasababisha uharibifu wa misitu.
"Lakini pia kumekuwa na uchomaji moto unaosababishwa na mila potofu na uwindaji haramu wa wanyama wakubwa na wadogo bila kujali madhara ya mioto wanayochoma,"alisema Tindikali.
Pia alitaja uvunaji wa mazao ya misitu kwa kutumia misumeno ya moto(chain saw) ni tatizo jingine linalotishia uhai wa misitu katika wilaya hiyo. Akibainisha mwaka uliopita walifanikiwa kumakata misumeno 25, iliyokuwa inatumika kuvuna mzao ya misitu. 

Ambapo pia alitoa rai zoezi la utengenezaji wa madawati lisitumike na watu wachache kujinufaisha.
"Wapo wajanja wa chache ambao wanatumia zoezi hili kuvuna mbao, tena kwa cheni so, hata hivyo mbao hizo hazipelekwi na kutumika kutengeneza madawati," aliongeza kusema.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo, Rukia Muwango, alimtaka ofisa elimu wa halmashauri ya wilaya, kuingia mikataba na walimu wakuu wa shule zitazikabidhiwa madawati ili wayatunze vizuri.

Pindi ukitokea uharibifu katika madawati watayokabidhiwa wawajibike kulipa. Madawati hayo yatarajiwa kukabidhiwa kwa shule za msingi Nachingwa na farm. 8. Ambapo wiki iliyopita, wakala huyo katika wilaya ya Kilwa ulikabidhi madawati 100 kwa mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top