Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: #TEKNOLOJIA :: REKODI YA KASI YA MTANDAO WA 4G KATIKA SIMU YAVUNJWA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Huku baadhi ya Makampuni nchini Tanzania yakipunguza Megabaiti za simu, jambo ambalo limelalamiki...
4G Connection
Huku baadhi ya Makampuni nchini Tanzania yakipunguza Megabaiti za simu, jambo ambalo limelalamikiwa na wateja wao wakidai kutokutendewa haki kwani matumizi ya Mtandao yamezidi kushika kasi.
fastest-4G Connection
Lakini Kampuni ya Finland Elisa inasema imefanikiwa kupata kasi ya Gigabaiti 1.9 kwa sekunde, ikisema hiyo ndio kasi ya juu zaidi kuwahi kupatikana.

Huduma hiyo ya simu yenye kasi zaidi inaweza kupakua Filamu ya Blu Ray kwa muda wa sekunde 44, lakini wachanganuzi wana wasiwasi kwamba kasi hiyo inaweza kutumika moja kwa moja katika mtandao halisi ulimwenguni.
Mobile
Elisa imesema kuwa imetumia teknolojia iliotolewa na kampuni ya China ya Huawei kutoa kasi ya upakuzi katika mtandao wa simu uliokaribia kiwango cha 2Gbps Ukilinganisha kasi yake ya mtandao ni 300Mbps ambayo iko chini mara sita.
Veli Matti Mattila
Mkurugenzi mkuu Veli Matti Mattila amesema, Tunajua kwamba hakuna kasi kama hii iliotangazwa na mitandao mingine.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top