Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: SIMBA SC YAMTUPIA VIRAGO JANVIER BOKUNGU NA KUMSAJILI MCHEZAJI HUYU HAPA
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Dar Es Salaam,Tanzania. Klabu ya Simba imemtema mlinzi wake wa kulia aliyesajiliwa siku za karibuni...
Dar Es Salaam,Tanzania.
Klabu ya Simba imemtema mlinzi wake wa kulia aliyesajiliwa siku za karibuni, Mcongo, Janvier Besala Bokungu baada ya kutoliridhisha benchi la Ufundi chini ya kocha mkuu, Joseph Marius Omog.

Janvier Besala Bokungu

Janvier Bokungu akikikabidhiwa jezi na picha ndogo kulia akitia saini wakati alipotua katika timu hiyo.

Simba imefikia maamuzi hayo na sasa nafasi yake inazibwa na Malika Ndeule ambaye rasmi amesaini Simba akitokea Mwadui FC na tayari jina lake lilishawasilishwa TFF kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano Tanzania bara.

Hata hivyo imefahamika kwamba nafasi ya Janvier Bokungu raia wa DR Congo huenda ikazibwa na Julius Ntambi wa URA ya Uganda.

Tangu awali kumekuwepo na taarifa kwamba kiwango cha Bokungu hakikuwaridhisha wengi ndani ya Simba ambapo walifikia hatua ya kumpa mkataba wa miezi sita huku wakiwa wanaendelea kutafuta mbadala wake.

Ntambi mwenye miaka 24 ndiye aliifungia URA bao la kwanza katika mchezo wa Fainali ya kombe la Mapinduzi dhidi ya Mtibwa mwezi Januari.

Simba bado wana nafasi ya kufanya marekebisho kwa wachezaji wao wa kigeni kwani dirisha la usajili kwa upande wa wachezaji hao halijafungwa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top