Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: SALUMU MWALIMU NA WENZAKE WA CHADEMA WARUDISHWA RUMANDE BAADA YA MVUTANO WA KISHERIA MAHAKAMANI
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Naibu katibu mkuu wa CHADEMA Tanzania visiwani, Salumu Mwalimu na wenzake 18 ambao ni wanachama wa ...
Naibu katibu mkuu wa CHADEMA Tanzania visiwani, Salumu Mwalimu na wenzake 18 ambao ni wanachama wa chama hicho wamefikishwa tena katika mahakama ya mkoa wa Simiyu,wakikabiliwa na mashitaka mawili ya kushawishi watu kuvunja sheria.
Salumu Mwalimu
Hata hivyo kesi hiyo haikutajwa mahakamani hapo baada ya kutokea mvutano wa kisheria baina ya wakili wa serikali mwandamizi, Yamiko Mlekano pamoja na wenzake sita ambao walikuwa wanaiwakilisha Jamhuri huku upande wa washitakiwa ukitetewa na wakili wa kujitegemea Godwin Simba.

Mbele ya hakimu mkazi mwandamizi mfawidhi wa mahakama hiyo John Nkwabi, wakili wa serikali Yamiko Mlekano amedai kuwa kwakuwa upande wa washitakiwa umechelewa kuwapa nakala ya majibu ya hati pingamizi ambayo waliiwakilisha jana mahakamani hapo ambapo upande wa serikali umeipata leo wakili huyo aliiomba mahakama hiyo iwape muda ili nao waweze kuisoma na kuijibu. 

Hoja hiyo ilipingwa na wakili wa washitakiwa kwa madai kuwa wao waliwakilisha hati hiyo jana mahakamani hapo na kwamba waliamini kuwa mahakama ndiyo yenye jukumu la kuwapa nakala upande wa serikali, Baada ya mvutano wa muda mrefu hakimu Nkwabi alitoa maamuzi ambapo alikubaliana na upande wa wakili wa serikali ambapo amewapa siku mbili kwa washitakiwa Salumu Mwalimu,Oscar Kaijage na Renatus Nzemo maombi yao ya rufaa yatasikilizwa tarehe moja mwezi wa 9 mwaka huu.

Aidha washitakiwa wengine 15 ambao kesi yao inasikilizwa na hakimu mkazi mfawidhi Mary Mliho mahakama imetoa siku moja kwa upande wa serikali kupitia hati pingamizi hiyo ambapo kesho kesi yao itaanza kusikilizwa ambapo washitakiwa wote 18 wamerudishwa gerezani.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top