Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: RPC - CUP LINDI KUENDELEA AGOSTI 21, 2016 HATUA YA NUSU FAINALI. TIMU ZAKABIDHIWA VIFAA LEO
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Diwani wa Kata ya Mnazi Mmoja Abdalah Mateva akipokea Seti ya Jezi kutoka kwa mratibu wa Mashind...
RPC - CUP 2016
Diwani wa Kata ya Mnazi Mmoja Abdalah Mateva akipokea Seti ya Jezi kutoka kwa mratibu wa Mashindano ya RPC - CUP 2016 Insp. Peter Msafiri, Makabidhiano hayo yamefanyika Leo Tarehe 20/8/2016 katika Ukumbi wa Maafisa wa Polisi Lindi. 
RPC - CUP 2016
Mratibu wa Mashindano ya RPC - CUP 2016 Insp. Peter Msafiri (katikati) akielezea jambo wakati wa makabidhiano ya Seti ya Jezi kwa Timu zilizofanikiwa kucheza Nusu fainali mashindani ya RPC - CUP 2016 leo Tarehe 20/8/2016 katika Ukumbi wa Maafisa wa Polisi Lindi. 
RPC - CUP 2016
Mwenyekiti wa Chama cha Marefa Ndg Athumani Sinani akielezea jambo wakati wa makabidhiano ya Seti ya Jezi kwa Timu zilizofanikiwa kucheza Nusu fainali mashindani ya RPC - CUP 2016 leo Tarehe 20/8/2016 katika Ukumbi wa Maafisa wa Polisi Lindi. 
RPC - CUP 2016
Mratibu Msaidizi wa Mashindano ya RPC - CUP 2016 Insp. Hamisi Andwilile (katikati) akielezea jambo wakati wa makabidhiano ya Seti ya Jezi kwa Timu zilizofanikiwa kucheza Nusu fainali mashindani ya RPC - CUP 2016 leo Tarehe 20/8/2016 katika Ukumbi wa Maafisa wa Polisi Lindi. 
RPC - CUP 2016
Viongozi mbalimbali wa timu zilizofanikiwa kucheza Nusu fainali mashindani ya RPC - CUP 2016 wakisikiliza kwa Makini maelezo ya waratinu wa Mashindano hayo leo Tarehe 20/8/2016 katika Ukumbi wa Maafisa wa Polisi Lindi.
(Picha zote na Fungwa Kilozo)

Na. Fungwa Kilozo, Lindi
Katika Kuelekea Hatua ya Nusu fainali ya Mashindano ya RPC - CUP Mkoa wa Lindi, Leo hii Timu zilizoingia hatua ya Nusu Fainali zakabidhiwa Jezi maalumu zitakazotumika katikaMashindano hayo katika hatua hiyo ya Nusu fainali na hatimae Fainali.

Akikabidhi Jezi hizo Insp. Peter Msafiri ambaye ndiye mratibu wa mashindano hayo amawataka viongozi wa Kata pamoja na Madiwani wa Kata zilizofanikiwa kuingia hatua hiyo kuzitunza Jezi hizo wakati wa Mashindano na Baada ya mashindano kwani amesema kuna tabia ya Timu kupewa vifaa na baada ya Mashindano wachezaji hujigawia na kufanya Timu hizo kukosa vifaa hivyo pindi watakapo kushiriki tena katika mashindano mengine, Hivyo aliwasisitiza kuwa atazifuatilia kwa karibu utunzaji wake.

Katika Hatua Nyingine Viongozi wa Timu pamoja na Bechi la Ufundi wamesisitizwa kufuata taratibu za Mchezo huo wawapo uwanjani, kumekuwepo kwa uvunjwaji wa kanuni kadhaa wakati wa Hatua ya Makundi hivyo wamesisitizwa katika hatua hii hakutakuwa na lelemama badala yake ni ufuataji wa sheria hizo.

Timu zilizofanikiwa kuingia hatua ya Nusu fainali ya RPC - CUP 2016 kwa kundi A ni Mnazi Mmoja akiwa ndio kinara wa Kundi hilo akifuatiwa na Mingoyo. Huku Kundi B likiongozwa na Makonde na Rasibura kushika Namba mbili.

Aidha Mchezo wa Kwanza wa Nusu fainali utachezwa Siku ya Jumapili kwa kuzikutanisha Timu za Mnazi Mmoja Vs Rasibura ambapo mchezo huo unatarajiwa kuanza mnamo saa 4:00jioni Ndani ya Uwanja wa Ilulu uliopo Manispaa ya Lindi.

Nusu Fainali ya Pili itapigwa siku ya Juma Tatu ikizikutanisha Timu za Makonde Vs Mingoyo, pia mchezo huo utaanza muda huo huo.

Insp. Peter aliweka bayana kanuni za hatua hiyo na kusema kuwa endapo Timu zitatoka sare basi dakika 30 zitaongezwa ilikutafuta mshindi na kama ikashindikana basi mikwaju ya penati itahusika kuamua nani Mshindi. Pia alisema katika Hatua ya Fainali hakutakua na dakika 30 za nyongeza badala yake mechi ikiisha mikwaju ya Penati itahusika moja kwa moja.

Aidha alibainisha kuwa zawadi ya mshindi wa Kwanza ni Kikombe, Medali ya Dhahabu pamoja na Pesa Kiasi cha Tsh 1,000,000.00. Huku Mshindi wa Pili atapata Kikombe Medali ya Fedha pamoja na Pesa Kiasi cha Tsha 600,000.00
na mshindi wa tatu yeye atazawadiwa kiasi cha Tsh 400,000.00 pamoja na Medali ya Shaba.

Zawadi nyingine ambazo zitatolewa kwa mchezaji mmoja mmoja Insp. Peter amesema kuwa kutakuwa na Zawadi ya mfungaji bora wa mshindano, Mchezaji chipukizi pamoja na kipa bora. Huku kikundi cha ushangiliaji kitakacho kuwa cha kwanza kitapatiwa Tsh 300,000.00.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top