Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: RPC CUP - 2016 LINDI:: RASIBURA YAICHAPA MNAZI MMOJA NA KUTINGA FAINALI
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Na. Fungwa Kilozo, Lindi Nusu fainali ya Kwanza ya Mashindano ya RPC - CUP 2016 yanayofanyika k...
RPC - CUP 2016
Na. Fungwa Kilozo, Lindi
Nusu fainali ya Kwanza ya Mashindano ya RPC - CUP 2016 yanayofanyika katika Mji wa Lindi ndani ya kiwanja cha ILULU yameendelea leo hii na Kuzikutanisha timu za Mnazi Mmoja Vs Rasibura.

Katika Mtanange huo ulioshuhudiwa na mashabiki lukuki kutoka katika kata mbalimbali zinazounda Manispaa ya Lindi na Kushuhudia Timu ya Rasibura ikitoa kichapo cha Goli 1-0 dhidi ya Mnazi mmoja.
RPC - CUP 2016
Mchezo huo ulianza kwa Tension kubwa kwa Timu zote mbili kwani Timu hizo hazijawahi kukutana kutokana na kuwa makundi tofauti na hivyo kuanza kwa kusomana kimchezo. Kitendo hicho kilichangia kutoonyesha soka la kuvutia kwa timu zote mbili.

Hadi Kipindi cha Kwanza kinaisha matokeo yalikuwa 0-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kushambuliana kwa zamu kwa timu zote mbili lakini ilikuwa na faida kwa upande wa Timu ya Rasibura kupitia kwa Mchezaji wake ambae aliingia kipindi cha pili na kufanikiwa kuibuka shujaa wa mechi hiyo Msafiri Kambwili kufunga goli pekee ambalo lilipeleka kilio kwa mashabiki wa Mnazi mmoja.
RPC - CUP 2016
Kesho Utachezwa Mchezo wa Pili wa Nusu fainali ya Mashindano hayo ukizikutanisha Timu za Mingoyo Vs Makonde. Mchezo huo utaanza kuchezwa saa 10.00jioni, Ndani ya Uwanja wa Ilulu.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top