Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: POLISI MKOA WA LINDI YAISAMBARATISHA SEMINA YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi Renatha Mzinga Na. Ahmad Mmow, Lindi. Kikao cha ndani cha ...
Renatha Mzinga
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi Renatha Mzinga

Na. Ahmad Mmow, Lindi.
Kikao cha ndani cha viongozi wa CHADEMA kanda ya Kusini kilichokuwakinafanyika Jana katika ukumbi wa Andrea Kagwa, Manispaa ya Lindi kimesambaratishwa na jeshi la Polisi ambapo viongozi hao wanashikiliwa na jeshi hilo.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa nane mchana, Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Lindi Seleman Methew alisema kikao hicho kilikuwa cha semina kwa ajili ya madiwani na viongozi wa mikoa na wilaya za Lindi na Mtwara. Iliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kujua wajibu, maadili na miiko ya uongozi ili wawezekuwahudumia vizuri wananchi katika maeneo yao. 

Akibainisha kuwa hakukuwa na lengo baya na kwamba kukodi ukumbi huo kwasababu ukumbi wa ofisi ya chama hicho usingetosha.
"Ni watu zaidi ya 40 kwakweli tusingetosha lakini jeshi la polisi na serikali isione kama kila jambo linalofanywa na upinzani ni bayakwani lengo la vyama vyote nikuwahudumia wananchi," alisema Methew.

Mwenyekiti huyo aliwataja viongozi wanaoshikiliwa na jeshi la polisi ni pamoja na Mwenyekiti wa Kanda ya Kusini, Hamisi Namangaya katibu wa kanda Filbert Ngatunga, Madiwani na viongzi wa wilaya na Mikoa ya Lindi na Mtwara wanaotokana na chama hicho.
"Hata mwezeshaji wa mafunzo aliyetokea na makamo meya wa manispaa ya Mtwara wamekamatwa," alisema Methew.

Nae katibu wa mkoa wa Lindi Mohamed Mahadhi alitupia lawama serikali kwa madai inavinyima vyama vya upinzani kufanya kazi na kutimiza wajibu wake uliopo kwa mujibu wa katiba na sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992.

Alisema hakukuwa na sababu ya jeshi hilo kuvuruga semina hiyo kabla ya kukutana na viongozi ili waelezwe lengo la semina hiyo. Katibu huyo aliongeza kusema kitendo kilichofanywa na jeshi hilo kinatoa picha kwamba wanachama wa chama hicho ni wakarofi.
"Pale vingeharibika vifaa na mali za wenye ukumbi tungeonekana CHADEMA ni wakorofi wameharibu mali,nikama vyama vya upinzani havihitajiki" alilalamika Mahadhi.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Lindi Renatha Mzinga bila kuingia kwa undani kueleza tukio hilo kutokana na jeshi hilo kuendelea na uchunguzi, alithibitisha kutokea tukio hilo.

Alisema miongoni mwa makosa ya viongozi hao ni kukusanyika bila kufuata taratibu na sheria (Bila ya Kibali).

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top