Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: PAUL MAKONDA ANENA HAYA JUU YA SEPTEMBA MOSI
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Septemba Mosi Mwaka huu ni moja ya siku ambayo imekuwa ikizungumzwa sana midomoni mwa watu kutokana...
Septemba Mosi Mwaka huu ni moja ya siku ambayo imekuwa ikizungumzwa sana midomoni mwa watu kutokana na mambo ambayo yamepangwa kufanyika siku hiyo, huku mengine yakitajwa kuwa na dalili za kuvuruga amani na mengine kuwa ya kihistoria na yenye tija kwa Taifa hili.
Paul Makonda
Moja ya mambo hayo ni Waziri Mkuu kuhamia Dodoma, Kupatwa kwa Jua, Maadhimisho ya Miaka 52 ya Jeshi la Wananchi, na Maandamano ya nchi nzima ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Katika kuelekea Septemba Mosi Matamko mbalimbali yawekuwa yakitolewa ambapo siku ya leo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameizungumzia siku hiyo na kueleza kuwa siku hiyo inatija sana katika historia ya Taifa hili kwani Jeshi la Wananchi linatimiza miaka 52 na siku hiyo jeshi hilo litakuwa lina usafi maeneo mbalimbali na kuchangia damu.
Paul Makonda
Kuatia maelezo hayo ya Mkuu wa Mkoa kuhusu Septemba Mosi aliulizwa kuhusu Maandamano ya UKUTA kufanyika siku ambayo wanajeshi watakuwa wanafanya usafi, ambapo Mkuu huyo wa Mkoa ameeleza kuwa “UKUTA ni kiwango cha mwisho cha mtu kufikiri”, hivyo hawezi kuwazungumzia watu ambao wamefika mwisho kufikiri, kwani kuna msemo wa kiswahili unasema amegonga UKUTA ikiwa na maana ya kuwa akili zake zimeisha.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top