Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: NAY WA MITEGO ANENA HAYA BAADA YA KUFUNGULIWA NA BASATA, ASEMA ATAENDELEA KUWACHANA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Baada ya Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) kumfutia kifungo cha kutojishughulisha na kazi za sanaa ...
Baada ya Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) kumfutia kifungo cha kutojishughulisha na kazi za sanaa msanii wa rap Tanzania, Nay wa Mitego na kumweka chini ya uangalizi maalumu, msanii huyo amedai kuwa ataendelea kuwachana watu kwenye nyimbo zake kama ilivyozoeleka.
Nay wa Mitego
Akiongea kwenye kipindi cha Funiko Base cha radio 5, Nay amesema kuwa ametumia muda mrefu sana kuwapata mashabiki wake hivyo hawezi kujiwekea mipaka kufanya anachotaka na kudai ataendeleza staili yake ya kuimba ila atafuata maadili zaidi.
“Leo nimemaliza matatizo na BASATA kwa hiyo ni Good Time kwa mashabiki wangu, kitu ambacho ninawaahidi ni kwamba nitaendelea kuwachana kama kawaida, tutapiga muziki mzuri kama kawaida ijapokuwa hatutavuka mipaka kuwakera watu wengine” 
Alifunguka Nay ambaye pia amesherekea kumaliza kifungo kwa ngoma mpya inayoitwa Good Time. IPAKUE KWA KUBOFYA HAPA

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top