Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: NAY WA MITEGO AKIFUATA NYAYO ZA SHILOLE ANAWEZA KURUDI KWENYE GAME, BASATA WAFUNGUKA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Kama unakumbuka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) lilitangaza kumfungia msanii wa bongo fleva Shilo...
Kama unakumbuka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) lilitangaza kumfungia msanii wa bongo fleva Shilole kutokana na sababu za kinidhamu hapo mwaka 2015, lakini msanii huyo amekuwa akionekana kuendelea na shughuli za sanaa tofauti na agizo hilo.
Shilole
Alipoulizwa kuhusina na Suala hilo kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio katibu wa BASATA,Bw. Godfrey L. Mngereza amedai kuwa Shilole alifuata taratibu zote alizotakiwa na baadaye kukata rufaa kwenye ngazi kubwa zaidi na adhabu yake ikaisha.
Nay wa Mitego
“Unajua sio kila kitu baraza tunatangaza,suala la Shilole ni kwamba alifuata taratibu na kwenda ngazi zingine na kukata rufaa kwa hiyo ilifikia huko na kumalizwa” alisema katibu huyo wa BASATA ambapo hivi karibuni wametangaza kumfungia msanii wa Hip Hop Nay wa Mitego.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top