Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: NAY WA MITEGO AFUNGUKA JUU YA KUBADILISHA STYLE YAKE YA UIMBAJI, ASISITIZA VIDEO YA PALE KATI PATAMU KUTOKA HIVI KARIBUNI
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Msanii wa hip hop Tanzania, Nay wa Mitego ambaye hivi karibuni amefungiwa na BASATA kwa muda usi...
Msanii wa hip hop Tanzania,Nay wa Mitego ambaye hivi karibuni amefungiwa na BASATA kwa muda usiojulikana kwa kutoa wimbo usiokuwa na maadili amefunguka na kusema kuwa hawezi kubadilisha aina ya muziki anaoufanya.
Nay wa Mitego
Akizungumza kwenye kipindi cha Ladha 3600 cha EFM,Nay amedai kuwa amekuwa akifanya muziki unaoleta changamoto kwa jamii kwa miaka 10 sasa ,hivyo kuamua kubadilika ni kuamua kuwapoteza mashabiki wake na kuweka wazi kuwa atajaribu kuepuka tu baadhi ya vitu ila sio kubadilika kabisa.
“Mimi nadhani mwandishi hapangiwi cha kuandika,na msanii anafanya kitu anachohisi ni biashara kwake..Mimi nafanya muziki wa aina hii mwaka wa kumi sasa,leo wewe ukiamua unataka mimi nibadilike basi uwe umeniandalia biashara nyingine ya kufanya ambayo itanipa kipato, na sio kirahisi hivyo,nina mashabiki wanaopenda ninachofanya.Kitu cha kujiuliza ni kwamba nimefanya muziki kwa miaka kumi Why leo? na nyimbo za nyuma zilikuwa na maneno makali zaidi.Ki ukweli kabisa siwezi kubadilisha muziki wangu ila kuna vitu tu nitajaribu kuviepuka”
Amefunguka Nay huku akisisitiza kuwa video ya kwanza ya wimbo wa Pale Kati ipo karibu kutoka.


*****************************************************

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top