Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI ANENA HUU SI WAKATI WA MAJADILIANO
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju , amesema huu si wakati wa kukaa katika meza ya ma...
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju, amesema huu si wakati wa kukaa katika meza ya majadiliano, hivyo viongozi wa dini watumie njia ya maombi kuliombea Taifa lisiingie kwenye uvunjifu wa amani kutokana na Operesheni Ukuta iliyoanzishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
George Masaju
Kauli hiyo ya Masaju imekuja siku chache baada ya Taasisi ya Maridhiano inayoundwa na viongozi mbalimbali wa dini nchini kutaka Serikali na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kukaa chini kutafuta suluhu ya mvutano unaoendelea kuhusu operesheni ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (Ukuta), ili kuepusha vurugu zitakazojitokeza nchini wakati maandamano hayo yaliyopangwa kufanyika keshokutwa.

Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Mchungaji Osward Mlay wiki iliyopita alisema ili kuepuka machafuko yanayoweza kutokea wakati wa kutekeleza operesheni hiyo Septemba mosi, mwaka huu huku Jeshi la Polisi lilisema litauvunja Ukuta ni vyema pande zote mbili zikajadiliana na kupata mwafaka.

“Hakuna jambo lililoshindikana mezani. Sisi kama taasisi ya maridhiano, tunaiomba serikali ikae mezani na viongozi wa Chadema ili kumaliza tofauti hizo,” alisema.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Masaju alisema viongozi wa dini wasing’ang’anie majadiliano bali wawashauri waumini makanisani na misikitini kutoshiriki kuvunja amani.

“Viongozi wa dini wanaweza kuendelea kufanya maombi dhidi ya hofu inayokuja na Ukuta, dhidi ya hali ya kutoheshimu sheria, warumi 3: mstari wa 17 -20 inasisitiza umuhimu wa kutii mamlaka. Ina maana hizo mamlaka ni Mungu. Kwa hiyo mtu akiiba anakamatwa na serikali. Si Mungu. Licha ya kuzungumza natoa option (njia) ya pili wanaweza kuangalia kuitii mamlaka iliyopo. Wasipojadiliana wakiacha kwenye hii nyingine ya maombi nchi ikiingia kwenye uvunjifu wa amani hali itakuwa mbaya.

“Suala la amani na utulivu haikuwekwa kwenye mamlaka mtu mwingine zaidi ya Rais, haya mambo ya siasa yanaweza kusababisha kusiwepo na usalama, kwenda kujadiliana naye maana yake unakwenda kuvunja Katiba na sheria,” alisema.

Alisema hakuna udhibitisho unaowalazimu viongozi wa dini na wa vyama vya siasa na Serikali kwa sababu polisi wanajua vitendo vya uvunjifu wa amani.

“Nyumbani nina Koran na Biblia, ninatambua umuhimu wa taasisi hizo za kidini, natambua wanasisitiza kufanya majadiliano, ila wawaambie waumini wao kuheshimu mamlaka hiyo ili kepusha shari, heri wapatanishi maana wataitwa wana wa Mungu, moja ya kupatanisha ni kuwaambia achana na haya, tunabaki wamoja."

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top