Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: MR.T TOUCH YAMEMKUTA HAYA BAADA YA KUTOKA KWENYE STUDIO YA NAY WA MITEGO
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Mtayarishaji wa muziki wa bongo fleva , Mr.T Touch ambaye alikuwa akifanya kazi kwenye studio za F...
Mtayarishaji wa muziki wa bongo fleva ,Mr.T Touch ambaye alikuwa akifanya kazi kwenye studio za Free Nation zilizo chini ya msanii Nay wa Mitego ametaja changamoto aliyokutana nayo baada ya kuachana na studio hizo.
Mr.T Touch
Akiongea kwenye kipindi cha Daladala beats cha Magic fm. Producer huyo amedai kwamba licha ya kuwa na mipango ya kuwa na studio zake,tukio la yeye kuondoka free nation lilikuwa la ghafla kwa hiyo hakuwa amejipanga vizuri hivyo kumgharimu mpaka pesa zake za akiba ili kuisimamisha studio yake mpya ya Touchez Soundz.
“Changamoto ziko nyingi,unajua kile kitu kilitokea ghafla ,japo ni kitu nilichopanga kuwa nacho(studio) ila ilibidi nikifanye haraka kutokana na mazingira yaliyotokea,kama unavyojua mtu unatumia hela hujui utairudishaje,labda unakuta una hela benki inabidi uitoe yote ili kufanyia vitu kama hivyo lakini najipanga” alifunguka T Touch ambaye amefanya hits kali kama Too much ya Darassa na Komela ya Dayna Nyange.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top