Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: MOTO WATEKETEZA BWENI BABATI, WANAFUNZI WAWILI WAPOTEZA FAHAMU KWA MSHITUKO
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Wanafunzi 80 wa shule ya sekondari ya Aldersgate inayomilikiwa na Kanisa la Mungu iliyopo katika Ha...
Wanafunzi 80 wa shule ya sekondari ya Aldersgate inayomilikiwa na Kanisa la Mungu iliyopo katika Halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara wamenusurika kuteketea kwa moto baada ya moto kuzuka na kuteketeza bweni, samani na vitu mbalimbali mali ya wanafunzi hao, ikiwa ni siku moja kabla ya uongozi wa shule hiyo kuifunga kwenda likizo ya muda mfupi.

BWENI LAUNGUA
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakizungumzia tukio hilo lililozusha taharuki iliyochangia wanafunzi wawili kupoteza fahamu na kulazwa katika hospitali ya Mrara ya Halmashauri ya mji wamedai hawatambui chanzo cha moto huo kuteketeza mali zao, lakini pia wakilaumu kuchelewa kwa askari wa jeshi la zimamoto huku mkuu wa shule hiyo Bw Dillo Fredson akidai chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme.

Nae Kamanda wa Jeshi la zimamoto mkoani Manyara Bw Heriel Kimaro amesema licha ya kutumia lita 12,000 kuzima moto huo kwenye bweni hilo lenye vyumba vitano amedai kushangazwa uongozi wa shule hiyo kuchelewa kutoa taarifa mapema kwa kupiga simu na.114 waliyokuwa wameitoa kwa uongozi huo.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi mkoani Manyara Afande Francis Jacob amethibitisha kutokea kwa tukio hilo usiku lakini amedai watalazimika kuwahoji mlinzi na mlezi ili kujiridhisha na endapo itabainika kuzembea watafikishwa kizimbani kwani majeshi yote mawili zimamoto na polisi walishatoa elimu na maelekezo ya majanga ya moto.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top