Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: MBWANA SAMATTA AIONGOZA KRC GENK KUPATA SARE DHIDI YA LOKOMOTIVA ZAGREB (+VIDEO)
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Mechi za kwanza Raundi ya Mwisho ya Mchujo zimechezwa hii Leo na Genk ya Ubelgiji, ambayo Straika w...
Mechi za kwanza Raundi ya Mwisho ya Mchujo zimechezwa hii Leo na Genk ya Ubelgiji, ambayo Straika wa Tanzania, Mbwana Samatta yumo, ilicheza ugenini huko Stadion Kaizerica Jijini Zagreb Nchini Croatia na Lokomotiva Zagreb ya Croatia na kutoka Sare 2-2.
Mbwana Samatta
Hadi Mapumziko, Genk walikuwa mbele 1-0 kwa Bao la Penati ya Dakika 35 iliyopigwa na Leon Bailey.

Kipindi cha Pili, Mbwana Samatta alitikisa wavu Dakika ya 47 na Timu yake Genk kuongoza 2-0 lakini Lokomotiva Zagreb wakazinduka na kusawazisha Bao zote Dakika za 52 na 59 Wafungaji wao wakiwa Mirko Maric, kwa Penati, na Ivan Fiolic. Hadi sasa Samatta ameweza kuifungia jumla ya Magoli 8 tangu alipotua kunako klabu hiyo akitokea TP Mazembe.

Hadi mwisho matokeo ni Lokomotiva Zagreb 2 KRC Genk 2. Mechi za Marudiano za Raundi hii ni Agosti 25.

Washindi wa Raundi hii wataingizwa kwenye Droo ya kupanga Makundi ambapo Manchester United na Klabu nyingine 15 zitaanzia hapo.


TAZAMA VIDEO YA MAGOLI YOTE HAPA

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top