Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: MAPYA YAIBUKA KUFANYA VIBAYA KWA YANGA MECHI ZA KIMATAIFA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
INASEMEKANA kuwa chanzo cha wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa Yanga kufanya viba...
INASEMEKANA kuwa chanzo cha wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa Yanga kufanya vibaya ni wachezaji wake kutolipwa mishahara.
Yanga
Habari kutoka kwa baadhi ya wachezaji wa Yanga inayoshiriki michuano ya kimataifa zinasema hawajalipwa mishahara ya miezi miwili na hivyo wachezaji wamevunjika moyo.

Yanga haijapata matokeo mazuri katika mechi zake nne za Kombe la Shirikisho Afrika ambapo imepoteza mechi tatu na kutoka sare mechi moja.

Timu hiyo kwa sasa ipo kwenye maandalizi ya kucheza na Mo Bejaia ya Algeria katika mechi nyingine ya michuano hiyo itakayochezwa Agosti 13 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Akizungumzia hilo, Katibu wa Yanga Baraka Deusdedit alikanusha taarifa hizo akisema hakuna mchezaji ambaye hajalipwa.

Alisema hadi kufikia sasa hakuna mchezaji yeyote anayeidai timu hiyo na huo ni utaratibu ambao wamejiwekea siku nyingi wa kulipa mishahara mapema ili kuwaongezea ari ya kujituma na kupata matokeo mazuri kwenye za michuano hiyo.
“Kama wanadai basi labda ni mshahara wa mwezi ujao, lakini hadi sasa hakuna mchezaji ambaye hajalipwa mshahara wake na hizo ni taarifa ambazo zina mpango wa kutaka kutuvuruga, lakini sisi kama uongozi tupo makini na matokeo tunayoyapata tunaamini ni ya kimichezo na hayatokani na wachezaji wetu kucheza chini ya kiwango,”alisema Deusdedit.
Katibu huyo alisema zipo changamoto nyingi wanazokumbana nazo hivi sasa hadi kushindwa kufanya vizuri, mojawapo likiwa ni ugeni wao katika michuano hiyo, lakini wanafurahishwa na kiwango na jitihada zinazooneshwa na wachezaji wao hadi kufika hapo walipo.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top