Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: MAPENZI YANAWEZA KUMGHARIMU MAVUGO ASIITUMIKIE SIMBA SC
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Mshambuliaji wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo MSHAMBULIAJI wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo, hivi...
Laudit Mavugo
Mshambuliaji wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo

MSHAMBULIAJI wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo, hivi karibuni alionekana kama amelijaribu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kuvaa jezi zenye namba mbili tofauti kwenye Ligi Kuu Bara.

Katika mchezo dhidi ya JKT Ruvu uliofanyika Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Mavugo alivunja kanuni ya shirikisho hilo baada ya kuvaa jezi namba 11.

Hii ilikuwa namba tofauti na ile ambayo aliivaa kwenye mchezo dhidi ya Ndanda ambapo alivaa namba 9 ambayo ilisajiliwa kihalali kuwa ni namba yake.

Kutokana na hali hiyo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), Boniface Wambura, aliliambia Championi Jumatano kuwa, kitendo hicho cha Mavugo kuvaa jezi zenye namba mbili tofauti katika mechi mbili tofauti za ligi hiyo ni kosa kubwa, hivyo wanamchunguza na anaweza kuchukuliwa hatua.
“Mchezaji mmoja kutumia namba mbili tofauti katika ligi ni kosa kikanuni, kama Mavugo amefanya hivyo, basi atakuwa amevunja kanuni hiyo.
“Hata hivyo, kwa sasa siwezi kulizungumzia sana suala hilo kwa sababu bado halijanifikia mezani kwangu,” alisema Wambura kwa ufupi huku pia akisita kuweka wazi adhabu ambayo Mavugo anaweza kukumbana nayo baada ya kutenda kosa hilo.

Alipoulizwa Mavugo kuhusiana na suala hilo alisema: “ Binafsi sikujua kama ni kosa lakini ninachoweza kusema ni kwamba niliamua kuitumia jezi namba 11 na kuachana na namba 9 kwa sababu nilikuwa nikiipenda tangu zamani.”

Kwa mujibu wa kanuni ya 60 ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2016/17, inayozungumzia usajili wa wachezaji kupitia vifungu vya 11 na 12 vinalitolea ufafanuzi suala hilo.

Kifungu cha (11) cha kanuni hiyo ya 60 kinasema kuwa: “Kila mchezaji wa ligi kuu atatakiwa kuwa na namba moja ya kudumu ya jezi ya kuchezea iliyosajiliwa na klabu yake wakati wa maombi ya usajili wa wachezaji."

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top