Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: MANCHESTER UNITED YAINYUKA BOUNERMOUTH 3-1, JOSE MOURINHO AANZA KWA "MWENDO KASI"
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Wakicheza huko Vitality Stadium katika Mechi ya kwanza kabisa ya himaya mpya ya Jose Mourinho y...
Bournemouth Vs Man United
Wakicheza huko Vitality Stadium katika Mechi ya kwanza kabisa ya himaya mpya ya Jose Mourinho ya Ligi Kuu England, Manchester United waliitandika Bournemouth Bao 3-1 na kuamsha shangwe za Mashabiki wao kuimba 'Jose Mourinho' mwishoni.
Bournemouth Vs Man United
Man United walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 40 baada ya pasi ndefu ya Anders Herrera kuwahi na Beki wa Bournemouth Simon Francis ambae alitoa nyuma kumrudishia Kipa wake Boruc lakini Juan Mata kuinasa na Kipa Boruc kuokoa na kumgonga tena Simon Francis na kurudi tena kwa Mata aliefunga kilaini.

Bao hilo lilidumu Hadi Haftaimu.
Bournemouth Vs Man United
Kipindi cha Pili Dakika ya 59 Kepteni Wayne Rooney akapiga Bao la Pili kwa Kichwa baada ya Krosi ya Valencia kuunganishwa fyongo na Anthony Martial na kumkuta Rooney aliemalizia hadi wavuni.

Bao la 3 la Man United lilipachikwa na Mchezaji Mpya Zlatan Ibrahimovic katika Dakika ya 64 na kuwa Bao lake la kwanza kwa Klabu yake mpya.
Bournemouth Vs Man United
Adam Smith aliipa Bournemouth Bao lao pekee Dakika ya 69 na Mechi kwisha Bournemouth 1 Man United 3.

Mwishoni Man United walifanya mabadiliko kwa kumtoa Juan Mata na kumpa Mechi ya kwanza Henrikh Mkhitaryan na kisha akatolewa Anthony Martial na kuongizwa Morgan Schneiderlin na kufuata Wayne Rooney na kuja Memphis Depay.

Mechi inayofuata kwa Man United ni ya Nyumbani kwao Old Trafford Ijumaa ijayo dhidi ya Southampton ikiwa ni Mechi ya Ligi Kuu England.

Ligi Kuu England inaendelea hivi sasa kwa mtanange mkali huko Emirates kati ya Arsenal na Liverpool na Jumatatu ipo Mechi 1 kati ya Chelsea na West Ham United huko Stamford Bridge.

VIKOSI: Bournemouth: Boruc; Francis, Adam Smith, Steve Cook, Daniels; Surman, Arter, Lewis Cook; Ibe, Wilson, King.
Akiba: Federici, Gosling, Ake, Afobe, Gradel, Brad Smith, Grabban.
Manchester United: De Gea; Valencia, Bailly, Blind, Shaw; Fellaini, Ander Herrera; Mata, Rooney, Martial; Ibrahimovic.
Akiba: Romero, Rojo, Memphis, Carrick, Rashford, Mkhitaryan, Schneiderlin.

REFA: Andre Marriner

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top