Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: #MAHABA :: MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA ILI USIKIMBIWE NA MPENZI
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Mapenzi ni hisia zisizozuilika na huwa hazichagui wakati, umri, rangi, dini, ama kabila; na ndio ma...
Mapenzi ni hisia zisizozuilika na huwa hazichagui wakati, umri, rangi, dini, ama kabila; na ndio maana ikasemekana “penzi ni kikohozi kulificha huwezi”. Asilimia kubwa ya wanaume wamekuwa wakilalamikia kuachwa na wapenzi ama wake zao bila kufahamu nini wafanye ili kuweza kuzuia mambo haya.
black couple
Basi usikonde wala usisononeke kwa sababu Kona ya Mahaba ipo kwa ajili yako kukuweka sawa ili usiachike wala usikimbiwe na mpenzi wako.

MWONESHE/ MPE MAHABA
black couple
Wanaume wengi wanashindwa kuwa wakarimu na wabembelezaji kwa wanawake zao, waacheni waiite Tanga Mapenzi yalipozaliwa kwani ni ukweli usiopingika wanaume wa Kitanga wanajitahidi kwenye ‘kupetipeti’.

MSILIKILIZE
black couple
Asilimia kubwa ya wanawake wanapenda kusikilizwa na hii iwe ana haki au hana haki jenga tabia ya kumpa nafasi ya kumsikiliza na kumshirikisha kwenye maamuzi yako hii itamfanya ajione mwenye thamani kwako.

MRIDHISHE
white coupleKwenye tendo la ndoa hakikisha unamridhisha kadri ya uhitaji wake na ikiwezekana mpaka mwenyewe akiri kuwa ameridhika, kama usipomridhisha jiandae wenzio kukusaidia majukumu yako.

Ukiweza kuzingatia mambo haya makuu matatu basi utakuwa umetii kiu ya mpenzi wako na kamwe hata kukimbia kwa sababu msingi upo hapa, hayo mengine ni ziada tu.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top