Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: KIDOGO YA DIAMOND YAZIDI KUPATA SHAVU, DANCER HUYU AAMUA KUUFANYIA VIDEO ICHEKI HAPA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Ni muda wa kufurahia japo kwa kidogo tunachoendelea kukiona kinachotokea kwenye muziki wa Bongo Fle...
Ni muda wa kufurahia japo kwa kidogo tunachoendelea kukiona kinachotokea kwenye muziki wa Bongo Fleva kwa kupiga hatua baada ya wimbo wa Diamond ‘Kidogo’ kufika Ulaya na sasa ni zamu ya Amerika Kusini.
Diamond
Hii ni hatua kubwa kwa Diamond na muziki wa Bongo Fleva kwa ujumla ikiwa ni siku chache kupita wimbo huo aliowashirikisha mapacha wa P-Square kuingia kwenye playlist ya redio yenye heshima kubwa Uingereza, BBC Radio 1Xtra.


Dancer mmoja kutoka nchini Colombia anayetumia jina la Bboydavii kwenye mtandao wa Instagram amepost vipande viwili vya video akiwa anacheza wimbo wa ‘Kidogo’ wa Diamond.2 Parte 💯 I Love Dance ❤💘COLOMBIA  @diamondplatnumz #kidogo @teamdiamondplatnumz🇨🇴🇨🇴 💯💪 @africanmuzikmag ✔, ameandika Bboydavii kwenye video moja aliyoiweka kwenye mtandao huo.

 
Bboydavii ameonekana kuufuatilia zaidi muziki wa Afrika kutokana na kupost vipande vya dance za nyimbo nyingi za wasanii wakubwa wa huku ikiwemo ‘Collabo’ ya P-Square, ‘Kpono’ wa Wande Coal aliomshirikisha Wizkid, na nyimbo nyingine nyingi.

Siyo muziki wa Diamond pekee ulionekana kukubalika nchi nyingine kwani hata wiki chache zilizopita kundi linalojiita L’fishta la Morocco lilirudia wimbo wa Shetta ‘Shikorobo’ aliomshirikisha msanii wa Nigeria, KCEE.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top