Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: KAULI YA MANJI KWA WANA YANGA: "KAMWE SITAWAACHA!"
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
RIPOTI zimeibuka kuwa Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji ametoa nia yake ya kuendelea na wadhifa wake ...
RIPOTI zimeibuka kuwa Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji ametoa nia yake ya kuendelea na wadhifa wake klabuni baada ya kuzagaa taarifa kuwa atabwaga manyanga baada ya kuudhika na wapinzani huku pia ikidaiwa mmoja wa wazee wa Yanga, Akilimali, amesimamishwa na Klabu hiyo.
Yusuf Manji
MANJI, licha ya kuwa Kiongozi wa Yanga anaependwa sana, pia ndie Mfadhili mkuu wa Klabu hiyo kongwe Nchini tangu Mwaka 2006.

Wanachama wengi, wakiongozwa na Viongozi wa Matawi, Jana walitoa sapoti kubwa kwa Manji na kushinikiza Mzee Akilimali alienukuliwa akitoa kauli tata za kuleta upinzani kwa Manji asimamishwe au kufutwa Uanachama wa Yanga huku wakitamka hilo Baraza la Wazee ambalo Akilimali ni mmoja wa Viongozi wake halitambuliwi Kikatiba na Yanga.

Leo Mwenyekiti Manji amenukuliwa Mitandaoni akitoa ujumbe mzito unaoashiria kubakia Yanga.

KAULI YA MANJI:

"Waambieni Wana Yanga pamoja na vurugu zote na kashfa ninazopewa lakini nitaendelea kuwa upande wao ,na kamwe sitawaacha kwani nguvu yangu kubwa ipo kwa Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Yanga Afrika!"

HABARI ZA AWALI:
SAKATA LA MANJI KUJIUZULU: VIONGOZI WA MATAWI YANGA WAMLAANI AKILIMALI, WATAKA AFUKUZWE!
BAADA ya Jana kuzagaa stori kuwa Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji amejiuzulu wadhifa wake kutokana na kusakamwa na matusi kutokana na mapendekezo yake ya kutaka kuikodi Klabu hiyo kwa Miaka 10 ili aiendeshe Kibiashara, Leo zimeibuka Taarifa toka kwa Viongozi wa Matawi ya Klabu hiyo wakilaani wapinzani hao.

Viongozi hao wamemwandama Mzee Akilimali ambae anadaiwa ndie alieibuka kumpinga Manji na kutaka afukuzwe Yanga mara moja.

HII HAPA NI TAARIFA ILIYORUSHWA NA KIKUNDI KIMOJA CHA YANGA KIITWACHO 'NAIPENDA YANGA'

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top