Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: JE WEWE NI MTUMIAJI WA KUKU NA MAYAI YA KISASA? TAARIFA HII INAKUHUSU USIDHARAU ITAKUCOST
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa nchini, TFDA , imebaini uwepo wa kemikali zinazobakia kwenye...
Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa nchini, TFDA, imebaini uwepo wa kemikali zinazobakia kwenye mayai ya kuku na kuku ambao tayari wanaenda kuuzwa ambazo si salama kwa afya ya binadamu.
Ummy Mwalimu
Hayo yanebainika wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya washauri wa TFDA ambapo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, ameiagiza mamlaka hiyo kuchukua sampuli na kufanya vipimo ili wizara ichukue hatua na kunusuru afya za watumiaji wa vyakula hivyo.

Katika hatua nyingine, Mh. Ummy ameiagiza TFDA kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza kwenye viwanda vya dawa kwa kuwapatia wataalam ambao watahakikisha dawa zinazozalishwa nchini zina ubora, kwani hivi sasa zaidi ya asilimia 85 ya dawa zinanunuliwa nje ya nchi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya ushauri ambayo inaishauri wizara kutoka TFDA Dkt. Ben Moses amesema wameyapokea maelekezo ya waziri na watayatekeleza kwa kipindi kifupi kuanzia leo, hasa suala la usalama wa chakula na dawa kuzingatiwa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top