Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: HUU NDIO UKWELI WA HASCANA KUFUKUZWA KAZI KATIKA STUDIO ZA WANENE ENTERTAINMENT
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Muongozaji wa video Tanzania, Hascana amefunguka kuhusu tetesi zilizoenea kwamba amefukuzwa kazi k...
Muongozaji wa video Tanzania, Hascana amefunguka kuhusu tetesi zilizoenea kwamba amefukuzwa kazi kwenye studio za Wanene entertainment ambazo zilikuwa zinamsimamia katika kazi zake za uongozaji wa video.
Hascana
Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo,Hascana amesema kuwa yeye hajafukuzwa na studio hizo bali yeye ndiye amevunja mkataba wa kufanya kazi na studio hizo na kuamua kujitegemea baada ya kuona tayari ameshafanya studio hizo zijulikane ambapo ndio ilikuwa kazi yake kubwa.
“Wanene hawawezi kunifukuza kazi” alisema Hanscana, “ni kweli kwa sasa sifanyi kazi na Wanene,jukumu langu lilikuwa ni kufanya watu waifahamu wanene,kwa kuwa tayari imeshafahamika,jukumu langu nimeshakamilisha” aliongeza Hascana na kusema,"Nimeamua wakati huu kusimama kama Hascana lakini hatuna ugomvi wowote" na kuongeza kuwa mkataba wake ulitakiwa uishe mwakani lakini ameusitissha baada ya kuona studio hizo zina uwezo wa kusimama peke yake.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top