Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: HIVI NDIVYO FID Q ATAKAVYO SHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA KWA MWAKA HUU
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Msanii wa hip hop Tanzania,  Fid Q ambaye atasheherekea siku yake ya kuzaliwa Agosti 13, amesema h...
Msanii wa hip hop Tanzania, Fid Q ambaye atasheherekea siku yake ya kuzaliwa Agosti 13, amesema huenda ataitumia siku hiyo kuachia kazi mpya kwa mashabiki wake.
Fid Q
Katika moja ya mahojiano yake Fid Q amesema kuwa huenda mwaka huu akahadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kuachia ngoma mbili tofauti na kawaida yake ya kuachia ngoma moja kwa mwaka kwa kuwa ana mzigo mkubwa wa nyimbo zilizopo kwenye maktaba yake.
“Watu wangu watarajie kitu cha tofauti na tayari wanaijua tarehe, Agosti 13, tena stock inavyoonyesha huenda tukafanya double release, lakini tutatoa tu kwa sababu stock ni nyingi sio kwa sababu ya Presha ya soko, kwa sababu nimekuwa nikitoa ngoma moja kwa mwaka, nimegundua siku hizi watu wanaelewa haraka, kwa hiyo ninaweza kuwafanyia mbili kwa mpigo, huwezi jua” alifunguka Fid.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top