Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: HILI JIPYA KUTOKA INDIA, NIKOSA KUMWANGALIA MWANAMKE KWA SEKUNDE 14
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamelalamika kuhusu tamko la afisa mmoja aliyesema kuwa ni kinyume...
Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamelalamika kuhusu tamko la afisa mmoja aliyesema kuwa ni kinyume na sheria kumuangalia mwanamke kwa zaidi ya sekunde 14 katika jimbo la Kerala nchini India.
indian beauty girl
Hakuna sheria kama hiyo nchini India lakini afisa huyo Rishiraj Singh ambaye ni kamshna amesema kuwa kumuangalia mwanamke kwa mda mrefu kunaweza kukutia mashakani.

Watu mitandaoni wanauliza itakuwaje iwapo mwanamume atafunga jicho mara moja na kulifungua akimwangalia mwanamke wakiongezea kuwa huenda bei ya miwani ya kujilinda dhidi ya jua ikapanda.
indian beauty girl
Lakini wengine wanasema kuwa bwana Signh amezua hoja nzuri sana kuhusu usalama wa wanawake.
"Mtu anaweza kushtakiwa kwa kumuangalia mwanamke kwa sekunde 14”, alisema bwana Singh katika eneo la Kochi siku ya Jumamosi.

Tamko hilo lililofanywa katika kanda ya video limesambaa katika jimbo hilo na kuzua ucheshi miongoni mwa mitandao ya kijamii.

Source:BBC

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top