Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: HAMISA MOBETTO NI MTANZANIA PEKEE ALIYETAJWA KWENYE TUZO ZA STARGT ZA AFRIKA KUSINI, MPIGIE KURA HAPA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Hamissa Mobetto ni staa pekee wa Tanzania aliyetajwa kuwania tuzo za Starqt zinazofanyika nchini ...
Hamissa Mobetto ni staa pekee wa Tanzania aliyetajwa kuwania tuzo za Starqt zinazofanyika nchini Afrika Kusini.
Hamissa Mobetto
Mrembo huyo ametajwa kuwania vipengele viwili, Best Dressed Lady (hadi sasa ana 66% ya Kura zilizopigwa) na People’s Choice Awards (Hadi sasa ana 20% ya kura zilizopigwa).

Hii ni mara ya tatu tuzo hizo zinatolewa na huwatunuku mastaa wa Afrika kwa kazi wanazozifanya katika sekta za muziki, filamu, mitindo, michezo na zingine.
Hamissa Mobetto
“Ni kitu kikubwa, somehow kinakuwa kama kinakutikisa kidogo hivi kiakili kwasababu ukiwa mtu pekee kutoka kwenye nchi yako na mwanamke na unakutana na watu wengine, lakini kila kitu kitakuwa kheri na tuzo itarudi nyumbani,” Hamisa alimuambia mtangazaji wa ABM Radio ya Dodoma, Dj Rodger.

“Mimi ni Mtanzania pekee niliyepo kwenye hizo tuzo na nilichaguliwa na wao wenyewe wakaamua kuniweka kwa kuona ninafaa, kwasababu mnakutana na watu wa Kenya, South Africa, Uganda, na nchi nyingine mbalimbali. Kwahiyo kuwekwa tu pale inaonesha wanakuappreciate,” ameongeza.
Hamissa Mobetto
Mrembo huyo amewaomba mashabiki wake kumpigia kura kwa kwenda kubonyeza link iliyopo kwenye bio yake ya Instagram au unaweza Bofya Hapa.

Tuzo hizo zitatolewa September 10 nchini Afrika Kusini.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top