Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: HABARI ZA HIVI PUNDE:: CHADEMA WASITISHA MAANDAMANO YA UKUTA BAADA YA KUPOKEA MAONI KUTOKA KWA....!!
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesitisha maandamano ya UKUTA ambayo yalipangwa kufa...
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesitisha maandamano ya UKUTA ambayo yalipangwa kufanyika Septemba 1 (kesho) baada ya kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa viongozi wa dini.
UKUTA
Akiongea na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amesema chama kimeona kisitishe maandamano kwa muda ili kiwaachie viongozi wa dini watafute suluhu kuhusu suala hilo.

"CHADEMA tunaomba kuwatangazia watu wote kwamba tunahairisha mikutano ya kisiasa na maandamano yote kwa muda wa mwezi mmoja," alisema Freeman Mbowe


"Viongozi wa dini walituambia tupeni wiki mbili au tatu, sisi tukawaongeza nyingine moja, Wadau walitusihi tusitishe ila tusiache, tumepata wakati mgumu mno kufikia uamuzi huu" aliongeza kusema Freeman Mbowe.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top