Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: #EPL :: GUARDIOLA MWENDO MPERA MPERA, MANCHESTER CITY IKIILAZA STOKE 4 - 1
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Manchester City chini ya Guardiola wakiwa ugenini wameendeleza wimbi lao la ushindi baada ya kuifu...
Manchester City chini ya Guardiola wakiwa ugenini wameendeleza wimbi lao la ushindi baada ya kuifumua Stock City mabao 4-1.
Stoke City Vs Man City
Sergio Aguero na Nolito kila mmoja amefunga magoli mawili na kuipa City ushindi huo mnono na kuendelea kupambana kileleni na mahasimu wao Manchester United Chini ya Jose Mourinho.
Stoke City Vs Man City
Goli la Stoke City lilifungwa na Bojan Krkic.

KAULIZA MAKOCHA BAADA YA MCHEZO
Bosi wa Stoke City Mark Hughes amesema: “Penati zilikuwa muhimu, hasa ile moja ambayo ilikuwa dhidi yetu kwenye kipindi cha kwanza. Kuna mabadiliko makubwa sana ya sheria kwenye msimu huu wa ligi. Ilitutoa mchezoni kabisa.

“Penati yetu pengine kama ingekuwa msimu uliopita isingetolewa, lakini ilitusaidia kurudi mchezoni mpaka tulipofungwa goli la tatu na kutoka kabisa mchezoni kabisa. Lakini siamini kama matokeo haya yameakisi mchezo ulivyokuwa.

“Kiukweli kwa mwaka huu Man City ni klabu kubwa hasa, na hatukuweza kupambana nao kutokana na kasi waliyokuwa nayo.”

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema: “Nafahamu vizuri namna gani wachezaji walivyo na ubora, najisikia ni mwenye bahati kubwa kutokana na ubora wa wachezaji niliokuwa nao hapa.

“Wanacheza mpira kwa kasi, wanakaba, na leo tumecheza katika moja ya viwanja vigumu sana kwenye ligi hii. Imenisikitisha kidogo kwamba tumetengeneza nafasi nyingi kipindi cha pili lakini hatukuweza kumalizia vizuri".
Stoke City Vs Man City
VIKOSI: STOKE CITY (4-2-3-1): Given, Bardsley, Shawcross, Wollscheid, Pieters, Whelan, Imbula (Walters 72), Bojan, Allen, Arnautovic (Ramadan 88), Diouf 6.
Subs not used: Muniesa, Adam, Cameron, Crouch, Haugaard.
Booked: Shawcross, Bojan, Allen
Goal: Bojan, 49

MAN CITY (4-1-4-1): Caballero, Zabaleta, Otamendi, Stones, Kolarov, Fernandinho, Navas (Nolito 69), De Bruyne (Delph 88), Silva, Sterling, Aguero (Iheanacho 83).
Subs not used: Hart, Fernando, Clichy, Maffeo.
Booked: Zabaleta, Sterling, De Bruyne
Goals: Aguero (pen)27, 35, Nolito 86, 90

Referee: Mike Dean

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top