Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: DULLY SYKES AMKINGIA KIFUA HARMONIZE KUHUSU KUMUIGA BOSI WAKE DIAMOND, NA HIKI NDICHO ALICHOKISEMA....
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Msanii mkongwe wa Bongo fleva Tanzania, Dully Sykes amesema haoni kama Harmonize anafanana na Dia...
Msanii mkongwe wa Bongo fleva Tanzania, Dully Sykes amesema haoni kama Harmonize anafanana na Diamond kwenye kuimba kama watu wengi wanavyosema.
Dully Sykes and Harmonize
Akihojiwa kwenye kipindi cha Friday night live cha East Africa Television, Dully pia amedai kuwa sio vibaya kama Harmonize anafanana na Diamond kwa sababu ndiye aliyemkuza kimuziki kwani watu wakikaa pamoja kwa muda mrefu hufanana.
"Mimi nina sikio la muziki,Harmonize yuko tofauti,kwanza hajazaliwa na koo la Diamond. Lakini wanamfananisha Harmonize kwa sababu ameishi sana pamoja naye, lazima mtafanana, Hata mimi kuna wasanii nimeishi nao wana pozi kama mimi,pia Harmonize amefikishwa mbali na Diamond kama ataamua kumfuata anavyofanya sio mbaya.Wakati mwingine kuna ukweli kuwa anafanana na Diamond kwa sababu amekua kwa Diamond,sasa mnataka afanane na nameless au?"
Alihoji Dully Sykes wakati akitambulisha video yake mpya alivyofanya na Harmomize kwenye kipindi hicho kinachoruka kila ijumaa kuanzia saa tatu usiku.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top