Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: DC NGUBIAGAI ATUMA SALAMU KWA "MAFATAKI"
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai Na. Ahmad Mmow, Kilwa. Mkuu wa wilaya ya Kilwa...
Christopher Ngubiagai
Mkuu wa wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai

Na. Ahmad Mmow, Kilwa.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai ametoa onyo kwa wanaume wanaopenda kufanya mapenzi na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani humo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Ngubiagai ametoa onyo hilo leo mjinikilwa Masoko wakati anafunga kikao kazi cha waratibu wa elimu wa katana walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari kilichofanyika kwa muda wa siku mbili katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Kilwa.

Alisema miongoni mwa sababu zinazochangia kiwango duni cha ufaulu katika shule za msingi na sekondari katika wilaya hiyo ni utoro na mimbazinazosababishwa na wanaume wasio na busara wala utu wenye tabia ya kuwataka wanafunzi ambao baadhi yao wanaweza kuwa na umri unalingana nawa watoto wao.

Hivyo wajiandae kushughulikiwakikamilifu kwa mujibu wa sheria bila huruma. alisema katika uongozi wake amedhamiria kufuta aibu kwa wilaya hiyo kushika nafasi ya mwisho kwa ufaulu katika mkoa wa Lindi.

Alisema njia mojawapo ya kutimiza azima hiyo nikuziba mianya inayosababisha, ikiwamo mimba na utoro.

Pia aliwaonya walimu hao kuwa onyo hilo nilajumla kwa madai kuwa baadhi ya walimu wanatabia ya kuwatongoza na kushirikiana kimapenzi na wanafunzi wao.
"Hali hiyo haikubaliki na haivumiliki, naomba nipewe taarifa ninani wenyetabia hiyo ilinianze kuwashughulikia, kama unatamani sana wanafunzi basi mnunulie mkeo siketi na shati ili afanane na mwanafunzi" alisema Ngubiagai.

Aidha aliwataka wakuu wa idara mbalimbali kuwapa ushirikiano kwa kuwasikiliza na kuwapa huduma wanazoombwa na watumishi wanaowaongoza. badala ya kuwanyanyasa na kuwadharau.

Alibainisha kwamba watumishi wote ni sawa. Hivyo hakuna sababu ya mtu fulani kujiona mwingine, kwasababu ya madaraka.

Kwaupande wao baadhi ya walimu walisema miongoni mwa sababu zinazochangia ufaulu mdogo ni wazazi na walezi kutokuwa na mwitikio mzuri wa elimu. Hivyo hawatoi ushirikiano na walimu. 

Mwalimu Mussa Mtuta, ambae alizungumza kwa niaba ya washiriki hao licha ya kumuhadi mkuu huyo wa wilaya kumpa ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha kiwango cha ufaulu kinaboreka, alisema wazazi ni kikwazo katika kufikia malengo kwasababu hawathamini elimu.

Hata hivyo aliunga mkono onyo lililotolewana mkuu huyo wa wilaya kuhusu tabia ya baadhi ya viongozi watendaji kuwadharau na kuwanyanyasa wanaowaongoza.
"Mkuu umesema jambo ambalo wengine hawajawahi kusema, nikweli sababu nyingine ni kwamba walimu tunadharauliwa hatupewi ushirikiano wa kutosha na baadhi ya wakubwa wa wilayani." Alisema mwalimu Mussa.

Wilaya hiyo ni miongoni mwa wilaya zilizokuwa zinafanya vizuri, hata hivyo hali ilibadilika baada ya baadhi ya viongozi ambao walikuwa karibu na walimu na sekta ya elimu kuhamishwa na kupelekwa wasio na uchungu na elimu ambao walikuwa hawatoi ushirikiano na waliobaki ofisini tu.
"Hivi sasa kiwango cha ufaulu kimeanza kupanda, baada ya kuletwa ofisa elimu wa shule za msingi tuliyenae, tangu ahamie ufaulu unaongezeka kwa sababu anajituma nayupo karibu na walimu." alibainisha Mwalimu Mussa.

Pia mwalimu huyo ambae ni mratibu wa elimu kata ya Miteja, alitaja sababu nyingine ni kucheleweshwa kushughulikiwa madai yao na muda mwingine kutoshughulikiwa kabisa, huku akiongeza kusema kutopandishwa madaraja kunawakatisha tamaa na ari ya kufanya kazi baadhi ya walimu.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top