Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: BENKI KUU YA WAASA WANANCHI KUCHANGAMKIA MIKOPO
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Wananchi wakipata maelekezo kutoka kwa Maofisa wa Benki kuu walioshiriki maonyesho ya Kilimo Na...
Benki kuu Nane Nane 2016

Wananchi wakipata maelekezo kutoka kwa Maofisa wa Benki kuu walioshiriki maonyesho ya Kilimo Nane nane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.


Na. Ahmad Mmow, Lindi
Wananchi wameshauriwa kuchangamkia mikopo ili kuinua vipato vyao kiuchumi badala ya kuamini benki zipo kwa ajili ya watu maalum na wenye vipato vikubwa.

Ushauri huo ulitolewa Jana na mkaguzi wa mabenki wa benki kuu, Ephraim Mwasanguti katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi, yalipokuwa yanafanyika maonyesho ya nane nane kitaifa.

Alisema wakulima, wafugaji na wavuvi pia wananafasi kubwa ya kuzifanya shughuli wananzofanya ziwe na tija kwako na kuchangia pato la taifa, iwapo watazitumia kikamilifu benki kwa kukopahata vifaa na zana za uvuvi na kilimo.

Akibainisha kwamba zipo kampuni tatu za karadha ambazo mkopaji anaweza kukopa vifaa na zana za kilimo, ufugaji na uvuvi kwa masharti nafuu na rafiki. Alizitaja kampuni ambazo zinaweza kukopesha vifaa na zana hizo kuwa ni Salute Finance Limited, Alios Finance Limited na Equity for Tanzania.
"Mkopaji atakopeshwa baada ya kuingia mkataba na kampuni atapewa mtambo anaohitaji na atalipa kwa kampuni ambayo itakuwa mmiliki wa mtambo"
"Kipindi kifupi kabla ya kumaliza deni atakuwa na hiari ya kununua kabisa kwa bei ya chini kuliko inavyouzwa dukani au kumaliza deni na kurejesha kwa kampuni," alisema Mwasanguti.

Idadi ya Taasisi zinazotoa huduma ndogo ndogo za kifedha zimeongezeka, mathalani hadi kufikia mwezi Machi mwaka jana kulikuwa na benki za biashara 22. 

Hata hivyo hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu idadi ya benki hizo za Biashara ziliongezeka na kufikia 36, ambapo mwaka jana jumla ya shilingi bilioni 90.8 zilitolewa kwa wateja 152,686.00. 

Ambapo hadi kufukia mwezi machi mwaka huu zimetoa asilimia 34 ya udhamini ulitolewa chini ya mfuko wa udhamini wa mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wakati (SME-CGS).

Aliongeza kusema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya udhamini uliotolewa chini ya mfuko wa Udhamini wa mikopo kwa ajili ya mauzo nje ya nchi (ECGS) ulikuwa ni kwenye mikopo ya pembejeo na miradi ya kilimo.

Akibainisha kwamba kupitia mfuko huo benki zimeweza kuvikopesha vyama vikuu vya ushirika na vyama vya msingi vinavyojishughulisha na ununuzi wa mazao na pembejeo za kilimo kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani.
"Hii imewezesha mfumo wa stakabadhi ghalani kupanuka na kufanya vizuri" aliongeza kusema.

Aidha Mwasanguti alieleza ongezeko la mabenki, alisema hadi mwezi marchi mwaka huu zimeongezeka na kufikia 63 kutoka 57 zilizokuwepo mwaka jana.

Ambapo matawi yameongezeka kutoka 698 yaliyokuwepo mwaka jana, nakufikia 732 hadi mwezi machi mwaka huu.

Ofisa huyo wa benki kuu alitoa wito kwa wananchi kutunza vizuri fedha, hasa noti ilikuepuka kuchakaa haraka na kuongeza gharama za uendeshaji. Kutokana na utunzaji mbaya ikiwamo matumizi makubwa ya fedha tasilimu wanapofanya Miamala.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top