Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: AVEVA MIKONONI MWA POLISI, NAHIZI NDIO TUHUMA ZILIZOSABABISHA KUWEKWA CHINI YA ULINZI
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii zinadai kwamba, Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva a...
Taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii zinadai kwamba, Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva anashilikiwa na jeshi la poili kwenye kituo cha Urafiki.
Evans Aveva
Aveva anashikiliwa na polisi kwa kibali cha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU lakini bado haijafahamika moja kwa moja anakabiliwa na tuhuma gani.

Kamanda wa polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, ACP Chistopher Fuime amethibitisha kumshikilia rais wa klabu ya Simba na alipoulizwa ni tuhuma gani zinazomkabili kiongozi huyo wa juu kabisa wa wekundu wa Msimbazi alisema ni vizuri swali hilo wakiulizwa TAKUKURU.
“Kama unaweza labda ungewauliza watu wa TAKUKURU wanaweza wakajua ni lini uchunguzi wao utakamilika na lini watampeleka mahakamani. Sisi tunamshikilia kwasababu TAKUKURU hawana mahabusu binafsi, vinginevyo wangekuwanae kule na wangejibu maswali yote ambayo wananchi wanataka kujua,”
Amesema Fuime kamanda wa Mkoa wa kipolisi Kinondoni wakati anahojiwa na kituo kimoja cha radio cha jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wa TAKUKURU kupitia afisa habari wao wamesema:
 “Tunamshikilia, yupo kwenye mikono salama. Sisi tunaendelea na uchunguzi wetu, sheria inaturuhusu kufanya uchunguzi tunaruhusiwa kukamata, kupekuwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu,” 
amesema Musa Milaba afisa habari wa TAKUKURU.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top