Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: AVEVA AACHIWA KWA DHAMANA, KABURU NA DEWJI NAO WAITWA KUHOJIWA NA TAKUKURU
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
RAIS wa klabu ya Simba Evans Aveva pamoja na wajumbe wa kamati ya utendaji waliokuwa wakihojiwa n...
RAIS wa klabu ya Simba Evans Aveva pamoja na wajumbe wa kamati ya utendaji waliokuwa wakihojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU wameachiwa kwa dhamana huku wakitakiwa kuripoti tena kesho.
Aveva na kaburu
Viongozi hao wanahojiwa kwa tuhuma zinazosemekana kuwa ni rushwa na ukwepaji wa kodi baada ya kile kilichoelezwa kuwa fedha za mauzo ya mchezaji Emanuel Okwi ziliwekwa kwenye akaunti binafsi ya Aveva badala ya ile ya Simba kwa lengo la kukwepa kulipa deni la mamlaka ya mapato TRA.


Aveva alikuwa wa kwanza kukamatwa huku viongozi wengine wakipigiwa simu ili wafike ofisini hapo kwa ajili ya mahojiano ambayo yataendelea kesho.

Mbali na Aveva viongozi wengine walioitwa ili kuhojiwa ni pamoja na makamu wa Rais Geoffrey Nyange 'Kaburu', Kassim Dewji, Said Tully, Jasmin na mhasibu Amosi.

Hata hivyo Jasmine hakuhojiwa kwahiyo atalazimika kufika ofisini hapo kesho ambapo pia Amosi amepewa melekezo ya kuripoti saa 4 asubuhi huku Aveva yeye akitakiwa kufika saa 7 mchana.

Shauri hilo linasimamiwa na mwanasheria wa Simba Evodius Mtawala ambaye aliwahi kuwa katibu mkuu wa wekundu hao wa Msimbazi.*************************************

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top