Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: ARSENAL YAANZA VIBAYA LIGI KUU, YAKUBALI KIPIGO KUTOKA KWA LIVERPOOL
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Uwanja wa Emirates Jijini London ulikuwa na sherehe ya Magoli baada ya Bao 7 kutumbukizwa wakati Li...
Uwanja wa Emirates Jijini London ulikuwa na sherehe ya Magoli baada ya Bao 7 kutumbukizwa wakati Liverpool walipovunja gundu la kushinda Mechi 1 tu Nyumbani kwa Arsenal walipotoka kwa Bao 1-0 na kushinda 4-3.
Arsenal Vs Liverpool
Hii ilikuwa ni Mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England kwa Arsenal na Liverpool iliyoacha cheche kubwa na mwishowe kuwakasirisha Mashabiki wa Arsenal waliochomoka polepole Uwanjani kwao na kuuacha mtupu mwishowe huku wakimlaani Meneja wao Arsene Wenger.

Arsenal walianza Mechi hii kwa kishindo kwa kukosa Penati iliyotolewa baada ya Beki wa Liverpool Moreno kumwangusha Theo Walcott na Walcott mwenyewe kupiga na Kipa Mignolet kuokoa.
Arsenal Vs Liverpool
Lakini Dakika 1 baadae Walcott alirekebisha na kuipa Arsenal Bao katika Dakika ya 31 ambalo lilisawazishwa na Philippe Coutinho katika Dakika za Majeruhi za Kipindi cha Kwanza.

Hadi Mapumziko, Arsenal 1 Liverpool 1.
Arsenal Vs Liverpool
Liverpool walikwenda mbele kwa Bao 4-1 kwa Bao za Adam Lallana, Coutinho na Sadio Mane lakini Arsenal wakaja juu na kupata Bao 2 na Gemu kuwa 4-3 na kuwa mshikemshike.

Hata hivyo, Liverpool waligangamala na kulinda ushindi wao wa 4-3.
Arsenal Vs Liverpool
Ligi Kuu England inaendelea Jumatatu Usiku kwa Mechi 1 kati ya Chelsea na West Ham United huko Stamford Bridge.

VIKOSI: Arsenal: Cech; Bellerin, Holding, Chambers, Monreal; Elneny, Coquelin; Walcott, Ramsey, Iwobi; Sanchez.
Akiba: Gibbs, Wilshere, Ospina, Oxlade-Chamberlain, Cazorla, Xhaka, Akpom

Liverpool: Mignolet; Clyne, Lovren, Klavan, Moreno; Lallana, Henderson, Wijnaldum; Mane, Firmino, Coutinho.
Akiba: Manninger, Grujic, Can, Origi, Matip, Stewart, Alexander-Arnold.

REFA: Michael Oliver

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top