Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: AFANDE SELE MIKONONI MWA POLISI MJINI MOROGORO
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Msanii mkongwe wa muziki kutoka Morogoro, Afande Sele amedai anashikiliwa na jeshi la polisi mkoan...
Msanii mkongwe wa muziki kutoka Morogoro, Afande Sele amedai anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Morogoro kwa madai anagawa pesa kwa watu ili kuwashawishi wajitokeze katika maandamano ya UKUTA ambayo yamepigwa marufuku.
Afande Sele
Rapper huyo ambaye ni mwanasiasa na aligombea ubunge kupitia cha ACT Wazalendo katika uchaguzi uliyopita, amedai yupo mikononi mwa polisi toka jana.

“Huku ni kushindwa kama sio kufeli, toka jana nipo mikononi mwa polisi eti naambiwa nimeratibu mkutano wa UKUTA , nimechapisha T-shirt na kugawa fedha ili kesho watu waandamane, pia kuaandaa mkutano maeneo ya Msamvu.,” aliandika Afande Sele kupitia facebook yake.

Aliongeza, “Nina zaidi ya mwezi sijakaa maeeneo ya Msamvu zaidi ya kupita nikiwa naelekea mikoani tena nikiwa kwenye gari yangu. Ila hii aibu na fedheha kwa jeshi la polisi, maamuzi ya kukurupuka . Tusubiri,”
post
Hata hivyo tunaendelea kufuatilia taarifa rasmi kutoka jeshi la polisi la Morogoro kuhusu kukamatwa kwake.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top