Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA APIGA MARUFUKU UVUTAJI WA SHISHA
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepiga marufuku uvutaji wa Shisha. Ameliagiza jeshi la polisi kuf...
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepiga marufuku uvutaji wa Shisha.
Shisha
Ameliagiza jeshi la polisi kufanya kazi kuhakikisha ulevi huo unapotea kabisa ili kuwalinda vijana wanaoutumia zaidi.

Ametoa agizo hilo kwenye hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na madhehebu ya Shia nchini mwishoni mwa wiki. Limekuja siku moja tu baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda naye kupiga marufuku uvutaji wa kilevi hicho pamoja na vitendo vya ushoga na uvutaji sigara hadharani.

Mheshimiwa Majaliwa alidai kuwa Shisha ni kilevi ambacho huchanganywa na vitu vingine vikiwemo viroba na pombe zingine.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top